kideko
JF-Expert Member
- Feb 23, 2017
- 296
- 217
Mim ni kijana umri miaka 28, Nina mchumba wangu nipo nae kwenye mahusiano mwaka wa nne sasa. Ila Ana tatizo ambalo lilimuanza 2014, alipata bleed miezi miwili mfululizo. Akaenda hospital akapimwa akaambiwa Ana hormone imbalance. Akapatiwa dawa tatizo likaisha, lakini mwaka Jana tatizo limemrudia tena la kubleed frequently miezi miwili, akapewa dawa pia likaisha, kuanzia 2014 mzunguko wake wa hedhi umebadilika anapata hedhi baada ya miezi miwili. Lakini tulipima tukaambiwa mfuko wa uzazi Upo Sawa hauna shida. Sasa tumepanga kufunga ndoa mwezi wa kumi na mbili mwaka huu, Nilikua Ni naomba ushauri je! Anaeza kubeba mimba na kuzaa kwa hali hii alio nayo! Nataombeni msahada wenu wakuu.