N.K. ni nchi ya kidikteta kuliko nchi yoyote kwa sasa. Maamuzi yote yahusuyo nchi hufanywa na mtu mmoja tu - the supreme leader ambaye utwawala wake alirithi kutoka kwa baba yake (Kim Jong Il) ambaye naye alirithi kutoka kwa baba yake (Kim Il-Sung). Ni nchi ambayo neno demokrasia halimo kwenye kamusi zao kwa maana halisi ya kuli-practice zaidi tu ya kuwa sehemu ya jina rasmi la nchi hiyo - DPRK kama ilivyo kawaida ya unafiki kwa nchi au taasisi zinazojidai kufuata mlengo wa kikomunisti/soshalisti/ujamaa.
Tkirudi kwenye swali lako; N.K. imewahi kupigana vita na S.K. miaka ya 1950; vita ambayo ilileta maafa makubwa sana ya kibinadamu na uhasama wa ajabu baina ya mbili hizo pamoja na Marekani na Japan. Kuhusu matokeo ya hiyo vita, ni vigumu kusema nani mshindi. Vita iliishia kwa kuwekeana ukanda maalumu baina ya mipaka ya nchi hizo; ukanda ujulikanao kama demilitarized zone (DMZ) ambapo ni marufuku kwa nchi mojawapo kuingiza jeshi ndani ya ukanda huo. Hata hivyo, N.K. imekuwa mchokozi wa mara kwa mara dhidi ya mwenzake, US, na Japan.