Naombeni msaada please

Kwa kweli! Lakini ipo siku Mola ni mwaminifu milele
Amen: mkuu kuna wakati tunashindwa kujitafakari wenyewe ila tunatafakari ya wengne kijijini kuna fursa kubwa kuliko mjini maana unauwezo wa kuendesha maisha kwa garama ndogo na ukatengeneza mkwanja mrefu
 
Nenda kwenye makampuni ya ujenzi omba kazi ya usaidizi. Ukipata utaanzia hapo kuzichanga
 
60,000 ni kubwa mnao. Kwa mtaji wa Elfu tano unaweza kuishi.

Nunua unga wa ngano kilo mbili na mafuta na viungo vingine mnajua wenyewe. Anza kupika mandazi au kalimati au mafenesi yale yenye kitobo katikati.

Ongea na wenye maduka hata watatu uwe unapeleka Asubuhi jioni unaenda unachukua hela.

Haya na hilo huwezi watakuona hujasoma labda
 
Pole sana mkuu, ushauri wangu usirudie kosa 2020 siyo mbali okey?
 
Nashukuruni kwa ushauri ,,ila kumbukeni hali za vijijini kwetu hapafanani ,mimi kurudi kijijini kwa sasa sitaongeza chochote zaidi ya kuongeza burden tu !, kuna wengine wametoka vijiji vyenye ardhi nzuri na maeneo makubwa pia hali ya hewa nzuri na wengine tumetoka sehemu zenye tabu tupu ,.Najua wengi watabeza sababu hayajawapata..Japo hajatokea hata mmoja wa kunisaidia hata shilingi mia ila nawashukuru kwa maoni yenu,ndivyo tulivyo watanzania tulio wengi tunaongea na kurahisisha mambo tu ila kusaidiana kwa tangible things hakuna..Naomba mtaji mnisaidie wa 60000 tu ndugu zangu lakini mnasema tu easly nirudi kijijini na wakati nauli yenyewe ya kurudi kijijini kwetu ni zaidi ya huo mtaji.Asanteni Mungu awabariki
 
tupe mrejesho mkuu
 
Asee mimi natafta mfanyakazi wa hotelini kama unaweza nichek kupitia hyo kaz taratibu utakua unatunza mtaji kwa malipo utayokua unapata nichek kwa taarfa zaid
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…