Naombeni msaada, nimepooza kuanzia mabegani hadi miguuni kutokana na ajali

Olive 1010

Member
Aug 20, 2013
34
20
Naitwa Wanko Kapunda and i am a survivor. Mimi ni mtu wa kawaida sana. Ile aina ambayo kama hunitafuti huwezi kuniona. Aina ambayo anaenda shule, anafaulu kwa grade C, anapata kazi, anaolewa, anaishi na familia yake vizuri hadi mwisho. I thought i was gonna live a simple quiet life. But life itself had a different plan for me. A mission for me. A mission to explore when is the best time for human to say this is the end.

Mimi nimepooza kuanzia mabegani hadi miguuni kutokana na ajali. Maisha yangu yamekuwa ya kulala, kukaa na kutegemea msaada wa kufanyiwa kila kitu. Ni maisha magumu. Ni maisha yanayonyonya maisha ya watu wangu wa karibu kwa namna za kikatili. Ni maisha ambayo hayamhamasishi mtu kuitamani kesho. Hatahivyo sijutii kuwa hai. Na sitojuta kamwe kwasababu hii ni asante yangu kwa wote wanaonipenda.

Matokeo ya matibabu yalionesha ntahitaji miaka mingi ya mazoezi hadi ntakapopona kabisa. Leo hii ni mwaka wa nne tayari na hali yangu bado ni ya kulala na kukaa tu. BUT... im ready now. Nimeyapokea maisha haya mapya na niko tayari kupambana. I am going to use my life to challenge life. At the end of this difficult yet adventurous life, ill make sure to have the answer of "when is the best time to stop".

Sina mikono kwahiyo natumia ulimi kuandika. Nimeandika script ya movie ambayo baada ya kushindanishwa na Maisha Film Lab imeingia 15 bora. Kwahivyo natakiwa kwenda zanzibar kwa ajili ya mafunzo zaidi kabla mshindi mmoja hajapatikana. Ntatakiwa kuondoka kijijini kwetu TAREHE moja july. Mafunzo yatakuwa bure lakini gharama ya usafiri wangu na wasindikizaji wangu utakuwa juu yangu. kwasababu kukaa ni changamoto, ntatakiwa kupumzika Mbeya, halafu Dar kisha ntamalizia hadi zanzibar. Kutokana na hali yangu nahitaji wasaidizi masaa 24 kwahivyo ntaongozana na wasindikizaji wawili. Kwahiyo mchango ninao omba ni wa kunisaidia kusafiri mimi na wasaidizi wangu wawili kutoka Rukwa hadi Zanzibar na kurudi Rukwa. Na malazi ya wasaidizi wangu kuanzia tarehe moja hadi kumi na nne. Asanteni sana kwa kuniunga mkono.
•Airtel money - 0683886446
•M-pesa - 0755836896
1466529413663.jpg


 
habari, mi nimeguswa na issue yako, kiukweli binafsi sina uwezo wa kifedha kukusaidia, ila ningependa ukija unifahamishe ninauwezo wa kukupeleka sehemu mbalimbali (mfano kwenye media) kwa ajili ya kueleza tatizo lako huenda ukapata msaada, nitatafuta usafiri kwa ajili ya mizunguko hiyo (kwa uwezo wa Mungu hilo lipo ndani ya uwezo wangu) namba yangu cheki kwenye PM.
 
...nimejaribu kui share hii post yako kwenye account yangu ya fb, but nimeshindwa, so kama kuna namna naweza kuipata nifahamishe then mi nitakupa account yangu ili niipost, naamini hii itasaidia pia
 
Nimeguswa. Kama mods au wadau au kwa namna iwayo yeyote ile itathibitishwa kuwa habari ya kweli nitatuma mchango wangu.

Samahani dunia haiaminiki sana siku hizi inabidi kuwa makini. Pole na kila la kheri
 
Nimeguswa. Kama mods au wadau au kwa namna iwayo yeyote ile itathibitishwa kuwa habari ya kweli nitatuma mchango wangu.

Samahani dunia haiaminiki sana siku hizi inabidi kuwa makini. Pole na kila la kheri

tomaso
 
Ni maisha ambayo hayamhamasishi mtu kuitamani kesho. Hata hivyo sijutii kuwa hai. Na sitojuta kamwe kwa sababu hii ni asante yangu kwa wote wanaonipenda.
Daaah.... haya maneno mdogo wangu hakika yamenichoma sana. Well. If you were in my vicinity I would solace you with Jim Reeves' song "Accross the Bridge" which has the following chorus:

Across the bridge, there's no more sorrow
Across the bridge, theres' no more pain
The Sun will shine across the river
And you'll never be unhappy again.


I promise to contribute something through your contacts though I'll stay anonymous. God is for us all.
 
Back
Top Bottom