Nijuwavyo ndoa huwa ina vigezo 6, ambapo umri ni kimojawapo. Kuna herufi sita A = age, B = body structure, C = character, D = displine, E = education background, and F=family background.
Suala la umri linakuwa mbaya pale mmoja anapokuwa mkubwa sana kuliko mwingine. Kuna dhana ya kujisikia 'infilia' kwa sababu ya udogo wako. Yaani kuna mmoja anakuwa kama anaishi kwa baba au mama yake kwa vile mwenzie amemzidi sana umri.
Lakini kwa upande mwingine, mwanamke kuzidiwa umri na mwanaume imekuwa ndo kawaida, na hili limetokana na dhana kwamba kwa sababu ya uzazi, mwanamke anazeeka haraka kuliko mwanaume given that other facors are kept constant. hivyo ili wote wawe na muonekano unaofanana, basi ikachukuliwa kuwa mwanaume amzidi mwanamke kwa kiasi fulani. Na ndiyo maana leo hii mwanamke kuolewa na aliyemzidi umri inaonekana ni kawaida kuliko the other way round.