Hahaha,Dada yangu humu Jf siku zote usiseme hutaki matusi.
Kuna watu wanajulikana kwa kejeli humu watakuja utawasikia.
Ushauri wangu ni kwamba bado mdogo sana na fursa unayo.
Kwanza pata radhi za wazazi,kaanao chini ili uwape ushauri wa utakachofanyia maamuzi.
Tabia ya kurejea mtihani inatakiwa kichwa kiwe kimetulia kweli.
Maana mie kuna dada mmoja amerejea mitihani mpaka akapata mume huko huko,ameolewa na bado Credit moja hajaipata.
Na ukizingatia kwamba wewe Tayari umeishaijua pesa na umeingia kwenye ajira.
Kurejea mtihani inapendeza zaidi mara tu ya kufeli kisha unaunganisha,hapo kichwa kinakuwa vizuri.Au either kungekuwa na Shule maalim kama zilizopo Dar ambazo unatenga muda wa jioni kwenda kusoma na mchana unafanya yako,hapo angalau.
Wazazi wako watakuwa wanajua kwamba ulikuwa unapenda kusoma kama unavyosema wewe mwenyewe na ndio maana wametembea na akili yako na wazo hilo.
Ila tambua kwamba kuna watu wanapenda kusoma lakini ukweli ni kwamba kila wakisoma kichwani hakikai kitu,mie nina shemeji yangu alikuwa anapenda kusoma kupita maelezo,lakini kila akisoma bado uwezo unakuwa sio kabisa licha ya kwamba unamuona yupo busy na masomo,hii ni hekma ya mungu.
Wazo la pili ni kwamba Tambua kwamba unapenda nini,ili ujiunge na chuo kama VETA ili upate taaluma(Professional skils) ili iwe rahisi kujiajiri.Hii nahisi itakusaidia sana kama utakuwa mjanja wa kucheza na fursa