Naombeni Kujua namna ya Kupambana na Chumvi kwenye Ujenzi wa nyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni Kujua namna ya Kupambana na Chumvi kwenye Ujenzi wa nyumba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiresua, Sep 26, 2012.

 1. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  wadau,

  Mkoa wa Morogoro hasa maeneo ya manispaa, ujenzi umekuwa unagubikwa na fault ya nyumba kuathirika na chumvi inayosabishwa na aina ya madini yalio kwenye ardhi (soil properties resulted from the rocks that formed the soil). sasa naomba kwa wale wataalam wa ujenzi watusaidie, je mbinu gani za kutumia?


  Kwa wale waliotembelea Mkoa wa Moro, ukiangalia kwa makini kwenye kingo za kuta nje na ndani kunalika sana! na nyumba nyingine zimakatika viuno

  Asanteni sana
   
 2. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Chonde chonde badilli hiyo tittle; ujenzi wa NYUMA unlaeta maana ndiyo-siyo katika thread yako!
   
 3. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  hahahaha asante, nimecheka mpaka basi
   
 4. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #4
  Sep 26, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  .........yaani umekalia kucheka wakati utata hujauondoa !? mimi naweza kukusaidi ushauri kwenye kudhibiti chumvi ya "mbele" kwani sina uzoefu na chumvi ya "nyuma" ! samahani lakini !
   
 5. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  kwa mazingira ya morogoro fanya yafuatayo:-1-baada ya kuchimba msingi (foundation trench) na kushindilia vizuri tandika NGOZI ULAYA(Damp proof membrane) kufuata mle utakapopita msingi then jenga msingi wako mpaka level unayoitaka.2-kabla ya kuanza course za tofali tandika karatasi maalum la kuzuia unyevu(Damp proof course) ,nadhani huu ni ujenzi wa nyumba za kawaida.kama utafuata maelekezo hayo hakuna hyo chumvi wala magari utakayoona.na material yote hupatikana kwny hardwares shops na kama hujanielewa utaniuliza.karibu!
   
 6. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Bro ally, this is not fair kaka!! it was natural mistake!
   
 7. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Brother Mgaya thanks for the well informed piece of advice! wengine wantumia mawe kwenye msingi (stone foundation) badala ya Tofali, je kuna ufumbuzi wa tatizo hili utaopatikana na matumizi ya mawe?

  swali lingine ni kuwa, umeshauri kutumia damp proof membrane chini kabla ya kuanza kuweka zege/kuanza kujenga msingi, nadhani hii itazuiya chimvi/magadi yanayopanda vertical (right?) swali.... hakuna uwezekano wa chumvi/au magadi ku-move horizontal kwnye ukuta wa msingi itakaokuwa into contact with soil? kumbuka when it rains water moves with the minerals! how about that!!
   
 8. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Huu ushauri ni hakika. Tatizo hilo nililiona hata Dodoma. na nilipoongea na watu wenye fani zao za ujenzi wakanishauri, niweke DPC. Kwangu imesaidia sana. labda kama chumvi itatokea tena miaka ya baadaye
   
 9. snochet

  snochet JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 1,271
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mgaya D.W,the solution uliyotoa ni ya kweli kabisa,ila ni before construction,je kama umeshamaliza nyumba yako na ishaanza kuumuka ukuta unazuiaje?....nimeshajaribu kuweka waterproof cement,ikazuia kwa muda ila ilipoisha nguvu ndo ikazidi,ukipaka normal cement ndo bure kabisa...if there is an effective solution naomba pia muiweke.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. M

  MLERAI JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 673
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Asante kwa ushari wako Mgaya wengi tulikuwa tunaweka dampo proof peke yake chini hatutandiki kitu na magadi yalikuwa yanapanda.Na je nitafanyaje ili kuondoa magadi kwenye ukuta kwani tofali nilizojengea kuna kipindi zinapandisha magadi na kusababisha rangi badanduka na ukuta kuwa mweupe
   
 11. f

  filonos JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  hilo tatizo lipo sehem nyingi kama LINDI..TANGA..MIKINDANI NK.. wao wmeisha zowea wanatumia msingi hua wa MAWE na hawa tumi CEMENT hutumia CHOKAA kuanzia COZ 3 pale tumia Tofari na CEMENT
   
 12. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Wizara ya ujenzi ina maabara mikoani pote, hapa Dar es salaam inaitwa CML -Central Materials Laboratory.
  Kile unachotaka kujua utapata ushauri hapo.
   
 13. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  mimi natafuta wale wajuzi wa kuchora ramani za nyumba na hasa kama upo morogoro, maana nina kiwanja changu pale Kola na nataka nianze ujenzi sasa. kama mpo huku tafadhali ni- PM
   
 14. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  BANDUGU BADO NASUBIRI MSAADA ZAIDI! bRO MGAYA WAPI TENA!
   
 15. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  We ni kama mimi mi nimetatua tumia w.cement
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tumia white cement story kwisha na thread imefungwa, mtu akiendelea ban
   
Loading...