Emmanuel chaulaya
Mkuu kwenye CPU model wanazipa model number tofauti kulingana na specifications zenyewe za CPU jinsi inavyoweza kuhandle features za simu kama wifi,bluetooth, camera etc.
Maelezo ya rahisi kabisa ni kama vile wanavozipa majina samsung s4, s5 ili kutofautisha models, hizi CPU nazo zinatengenezwa na makampuni tofauti na wanaotengeneza simu,
simu yaweza kua Samsung, lakini CPU ikawa wamenunua mfano MediaTek au Intel kwa hiyo wanachagua model kulingana na uwezo wanaotaka...
GPU version Open GL ES 2.0, unajua GPU ni hardware unayoiunga kwenye kitu kama simu au computer au device yoyote ile kwa ajili ya graphics computation, kama simu mfano, haitambui GPU ni nini utakapoiunganisha, ndo hapo zinapokuja hizi API kama hii ya Open GL,
inafanya GPU ijitambue kua ni GPU na kazi yake ni kuprocess graphics, hizi API zinaruhusu mtu anayetumia GPU hiyo kuicommand anavyotaka kwa programming.
CPU na GPU hazifanani kwa kila simu, ingawa zipo kwenye kila simu, ndo maana simu kama Galaxy note 4 utakuta ni fasta kuliko note 2 sababu ina CPU ambayo iko faster zaidi,
au unaweza kuta unaangalia movies zenye very high quality 1080p+ kwenye note 3 lakini hiyohiyo movie ikashindwa kucheza bila kukwamakwama kwenye simu kama IDEOS, sababu GPU ya note 3 ni faster zaidi... Kwa hiyo unaponunua simu angalia CPU na GPU yake ni ipi, unaweza google online kuangalia CPU gani zina speed nzuri kuhandle task zote unazozitupia.