Naomba ushauri

Naomba ushauri

Konaball

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Posts
2,949
Reaction score
1,943
Miaka 10 iliyopita niliowa mke na nikazaa nae watoto wawili lakini baadae nikaachana nae, yeye akarudi kijiji kwao na kwa bahati akaolewa na mume mwingine na mimi nikaowa mke mweingine, mwaka jana mwezi novemba alikuja jamaa kupanga katika nyumba yangu na akasema mkewe amuacha kijiji kwao, mwezi huu amemleta yule mkewe na ndio yule mke wangu wa mwanzo. Naombeni ushauri je nimuamishe jamaa au niendelee akae pale na mkewe?.
 
Je ulimtelekeza??hukuwa na mawasiliano nae tena??...kwa nini unasita kumuacha akae na mumewe..??hatma ya watoto wenu vipi ???
 
Umuhamishe kwenda wapi?

Kama ulikuwa wampenda sana mkeo kilichokufanya umuache ni kipi?

Wakati wewe wasema wa nini, wenzako wajiuliza watampata lini...
 
Huyo sio mkeo tena kwa hiyo wewe chuna tu asijue mkeo wala mumewe kuwa mliwahi oana. Lakini kama una watoto wake unaishi nao hapo kazi.
 
Vipi unahofu unaweza kuomba tena mchezo? Kama ni hivyo warudishie kodi yao!
 
Hahahahaaaa....... Vipi, ni wivu unakusumbua braza?

Wewe uko na wako, nae yuko na wake... Tatizo liko wapi?

Hebu achana na mambo ya watu, kuwa bize na mkeo mpya..!! Lol
 
Kwa uandishi huu unaonekana bado ni hawa vijana wa teknohama...sijui ulipata wapi hela za kujenga nyumba ya kupangisha! Nakata simu...ooh sorry hivi mkataba wako uliweka kipengele kwamba akija mpangaji aliyemwoa mkeo mkataba unaishia hapo hapo?
 
Coincidence is another God's way of remaining anonymous...........

Ndo maza house karudi nyumbani kwake hivyo we mpokee tu kwa mikono miwili

Na kama ndoa yako ya pili inazingua basi lazima andiko litimie fasta
 
Umuhamishe kwenda wapi?

Kama ulikuwa wampenda sana mkeo kilichokufanya umuache ni kipi?

Wakati wewe wasema wa nini, wenzako wajiuliza watampata lini...

yeye ndio alieniacha
 
Je ulimtelekeza??hukuwa na mawasiliano nae tena??...kwa nini unasita kumuacha akae na mumewe..??hatma ya watoto wenu vipi ???

hapana watoto nilikuwa na wahudumia kama kawaida na kaja nao hapa nyumbani na mumewe
 
Kwa hekima ya kawaida, ni vizuri ukawa mbali nao.

Otherwise yafuatayo yatatokea
1) Mume wa huyo akijua huenda asiamini kuwa hamuendelei na ukizingatia yeye kapanga kwako, atajiona inferior na sio rahisi mawazo ya kuibiwa yakamuondoka japo yawezekana hata hayo mawazo huna.

2) Ukaribu wowote kati yako na hao wapangaji wako huenda ukatafsiriwa vinginevyo

3) Chochote ambacho utafanya kisichowapendeza (japo ni haki kifanyike) watakimbilia kusema unawakomoa au unalipiza kitu kwa huyo mwanamke (unawanyanyasa)

4) Baada ya muda huenda ukamlia mtu mkewe. (kuna konnection kubwa sana kati ya watu walioachana na wakazoeana tena lazima watakumbushia tu)

Ingekua mm baada ya mkataba huu kuisha ningewaomba wapange pengine kwa sababu yeyote ambayo itafaa kwa wakati huo.


Miaka 10 iliyopita niliowa mke na nikazaa nae watoto wawili lakini baadae nikaachana nae, yeye akarudi kijiji kwao na kwa bahati akaolewa na mume mwingine na mimi nikaowa mke mweingine, mwaka jana mwezi novemba alikuja jamaa kupanga katika nyumba yangu na akasema mkewe amuacha kijiji kwao, mwezi huu amemleta yule mkewe na ndio yule mke wangu wa mwanzo. Naombeni ushauri je nimuamishe jamaa au niendelee akae pale na mkewe?.
 
I like your statement.
Coincidence is another God's way of remaining anonymous...........

Ndo maza house karudi nyumbani kwake hivyo we mpokee tu kwa mikono miwili

Na kama ndoa yako ya pili inazingua basi lazima andiko litimie fasta
 
Ila mkuu, it is an obvious fact kuwa lazima kutakuwa na muingiliano kwenye hizo ndoa mbili. Kiutu uzima lazima solusheni ipatikane

Umuhamishe kwenda wapi?

Kama ulikuwa wampenda sana mkeo kilichokufanya umuache ni kipi?

Wakati wewe wasema wa nini, wenzako wajiuliza watampata lini...
 
Back
Top Bottom