Habari zenu wana JF
Mm ni mwanamke , nimelelewa vizuri na wazazi wangu wote wawili, nimesoma nina advance diploma ya IT na kwa sasa naongeza ujuzi wangu ktk chuo cha IFM.
Nimeolewa na nina watoto wawili, mume wangu wa kwanza tuliishi miaka 8 , kutokana na mateso na vitimbwi kwa kweli nilishindwa kuendela kuishi naye nikaondoka.
nikaenda kupanga na nikawa ninaishi na watoto wangu . nilipata shida kwa muda lkn baadaye nikazoea. ninachoshukuru mungu nilikuwa na kibarua changu .
baada ya kiniacha tu, nikasikia kuwa ameoa na anaishi na huyo mwanamke kwenye nyumba tuliojenga wote. iliniuma sana , nikaamua kumshukuru mungu .
siku moja katika kuhangaika tulikutana mjini, akaniangalia kuanzia juu hadi chini na kuniambia maneno ya kejeli kiasi nilitamani ardhi ipasuke niingie. niliumia sana ,
siku nyingine akaambiwa kuwa huwa nakwenda kwenye maombi akasema na bado nitachanganyikiwa sana. kwa kweli namshukuru mungu alinifungulia mlango nikapandishwa cheo kazini na nikapata kwenda kusoma .
katika kukaa kwa muda nikapata tena mwanaume mwingine nikampena sana na nikaolewa naye na nikazaa mtoto mmoja na tunaishi vizuri sana , katika muda wote huo yule mume wangu wa kwanza alikuwa hanijali wala nn na wala hakuwahi kuleta matumizi yoyote yale kwa watoto. lkn cha kushangaza leo hii anadai watoto. na na kunitishia kuwa atanipeleka mahakamani kuninyanganya watoto.
kwa kweli inaniletea shida sana na kunitesa moyoni tena na kukumbuka mateso yote aliyokuwa ananipa tulipokuwa tunaishi wote.
wanajamii naombeni msaada nifanye nini ?
yaani umenipigilia msumari wa moto moyoni mwangu , ungejua nilivyonyanyasika nao usingesema, halafu pia watoto wenyewe wa kike , si baadaye watakuja kuwa machangu , maana sina hakika kama watalelewa vizuri .
Nashukuru kwa ushauri wako.
hata mm nafikiri ni hilo la kutaka kuniharibia ndoa yangu ndilo analo kichwani kwake.
maana nilipoachana naye nilikwenda kupanga mbali kidigo naye lkn eneo ni hilohilo tegeta, basi siku moja alikuw anapita na agri mm nimebeba mtoto mgongoni asubuhi nampeleka hospitali. akaniona lkn hata kuniuliza hakuniuliza wala kunipa lift ili niwahi walaaaaa, akapita kama hanijui ihali mtoto ni wakwake, nililia sana asikuambie mtu, na sitakagi kukumbuka maana nahisi simanzi. lkn nashukuru akapita msamalia akanipa lift na pesa za matibabu. yaani nilipata shida mm anayejua ni mungu.
nitapigana na nitasimama kwa miguu yangu I PROMISE THAT.
wa kwanza yupo darasa la sita ana miaka 11
wa pili ana miaka 9 yupo darasa la nne
nyamayao nawapenda sana wanangu na nitapigana mpk damu ya mwisho kwa ajili yao. nilipokwa nakwenda kwenye maombi nilikuwa naomba mungu anibariki nilee watoto wangu wakue ili waje wanisaidie.
Pole sana dada yangu. Mimi ni mwanamume, imenisikitisha sana hii story yako. Nachotaka kukushauri ni kuwa (1) una kila haki ya kuishi na wano sawa na yeye alivyo na haki. Lakini ukijipanga vyema nionavyo mimi kimazingira wewe ndiye ambaye unafaa zaidi kuishi na hao watoto. Kama walivyotangulia kukushauri wadau wengine. Nenda TAMWA waeleze kinaga ubaga hali ilivyokuwa baada ya ninyi kuachana, na hadi hapo ulipofika na jinsi ambavyo watoto umewatunza bila shida na hofu yako ikiwa hao watoto wataenda ishi naye. Ni mambo ambayo yapo wazi kila mtu anajua kuwa watoto wengi wanaoishi na mama za kambo huteseka kuliko wale waishio na baba za kambo.(2) Wewe ni mwanamke, naamini kwa kuwa umekuwa na hao wanao kwa muda mrefu ni wazi wanakupenda na ni rahisi kuwafanya wakakukubali wewe kwani hata mkienda mahakamani watoto wakisema hawataki kwenda ishi na baba yao bali na wewe hawawezilazimishwa!! SO STOP CRYING WOMAN, SHOW HIM THAT YOU ARE STRONG! I TRUST IN STRENGTH F YOU WOMEN. May God be with you.
Habari zenu wana JF
Mm ni mwanamke , nimelelewa vizuri na wazazi wangu wote wawili, nimesoma nina advance diploma ya IT na kwa sasa naongeza ujuzi wangu ktk chuo cha IFM.
Nimeolewa na nina watoto wawili, mume wangu wa kwanza tuliishi miaka 8 , kutokana na mateso na vitimbwi kwa kweli nilishindwa kuendela kuishi naye nikaondoka.
nikaenda kupanga na nikawa ninaishi na watoto wangu . nilipata shida kwa muda lkn baadaye nikazoea. ninachoshukuru mungu nilikuwa na kibarua changu .
baada ya kiniacha tu, nikasikia kuwa ameoa na anaishi na huyo mwanamke kwenye nyumba tuliojenga wote. iliniuma sana , nikaamua kumshukuru mungu .
siku moja katika kuhangaika tulikutana mjini, akaniangalia kuanzia juu hadi chini na kuniambia maneno ya kejeli kiasi nilitamani ardhi ipasuke niingie. niliumia sana ,
siku nyingine akaambiwa kuwa huwa nakwenda kwenye maombi akasema na bado nitachanganyikiwa sana. kwa kweli namshukuru mungu alinifungulia mlango nikapandishwa cheo kazini na nikapata kwenda kusoma .
katika kukaa kwa muda nikapata tena mwanaume mwingine nikampena sana na nikaolewa naye na nikazaa mtoto mmoja na tunaishi vizuri sana , katika muda wote huo yule mume wangu wa kwanza alikuwa hanijali wala nn na wala hakuwahi kuleta matumizi yoyote yale kwa watoto. lkn cha kushangaza leo hii anadai watoto. na na kunitishia kuwa atanipeleka mahakamani kuninyanganya watoto.
kwa kweli inaniletea shida sana na kunitesa moyoni tena na kukumbuka mateso yote aliyokuwa ananipa tulipokuwa tunaishi wote.
wanajamii naombeni msaada nifanye nini ?
...Ohhh,
Mungu akupe nini! Mpe naye alee wanawe.
ilikuwa ni wajibu wake kuchangia malezi ya watoto,
kama ilivyo sasa anapotaka kuwachukua wanae awalee.
Usijitishe na doubts,...
Mpe kwa moyo mmoja, tena waambie watoto huyo ni baba yao,
nawe ni mama yao. Wana haki zote kwake na kwako pia.
Watoto hawana makosa.
La msingi, hakikisha mnakubaliana rights zote za kuwaona watoto,
iwe ni weekends, likizo, au kila baada ya muda fulani.
Incase watoto wanaathirika na mazingira, nyie wazazi wawili mkubaliane
watoto wapewe haki ya kuishi pale kwenye mazingira sahihi na makuzi yao.
Mbu huyu baba, mbona inaonekana hawezi hata kuwalea hawa watoto?
Kumbuka hapo, anaishi na mwanamke mwingine ambaye hana watoto/mtoto.
Mmmmh awe anayo hiyo neema ya kuwalea watoto wa mwenzie, vinginevyo,
watoto watakuwa watu wazima wenzie.
Ukiangalia historia ya huyu baba inatia mashaka kama ni kweli anawataka watoto kwa wema,
Kwa hiyo LD unataka kuniambia anawataka ili akawatie kwenye oven?
Otherwise uniambie we ni nabii, ila kiukweli baba naye ana haki ya kuwalea wanae.
Mbu huyu baba, mbona inaonekana hawezi hata kuwalea hawa watoto?
Kumbuka hapo, anaishi na mwanamke mwingine ambaye hana watoto/mtoto.
Mmmmh awe anayo hiyo neema ya kuwalea watoto wa mwenzie, vinginevyo,
watoto watakuwa watu wazima wenzie.
Ukiangalia historia ya huyu baba inatia mashaka kama ni kweli anawataka watoto kwa wema,
..naam LD, historia ya huyu baba kama tulivyohadithiwa na
mtaliki wake, dada yetu Lisa.
Kumbuka, mpaka sasa hatujapata upande wa pili wa shilingi,
maelezo ya Huyu baba, ili experiences zetu zi judge ukweli.
Character assassination ni jambo la kawaida baina ya wawili walioachana,
Sioni tofauti ya jambo hili hapa, ingawa kwa maelezo ya dada Lisa 'inaonekana'
kuna mapungufu ya hapa na pale kwenye judgements.
Kuna cases nyingi nazijua ambazo Mwanamke kwa kutumia kivuli cha haki za mtoto
ameweza kumnyima haki zake mwanaume kumuona/kuwaona watoto wake kiasi cha kupelekea
Uhasama mkubwa baina ya wazazi wawili na mtoto/watoto wao.
Ndio maana nasimamia hoja yangu, watoto ni haki ya wazazi wote wawili.
Huyo baba amekosa malezi ya watoto wake kwa miaka nane sasa,
Imagine, walipoachana (8yrs ago,) huyo mdogo alikuwa na 1yr na mkubwa 3yrs...
Kuna mushkeli mkubwa hapa.
Mheshimiwa Mosquito adui mkuu wa klorokwini lakini si Asprin, leo mi nna kazi moja tu kukugongea hii kitu:
The Following User Says Thank You to Mbu For This Useful Post:
Asprin (Today)
LD darling....Never rely on one sided story!....Hapa tungepata habari ya upande wa pili tungeweza kuhukumu. Kwa upande wangu, mme wa kwanza ataendelea kuwa innocent mpaka nitakapoisikia story ya upande wa pili.
Kumbuka wanaoachana, kila mmoja anamuona mwenziye ndo ana makosa!
Asante sana kwa kuguswa na tatizo langu , pia nashukuru sana kwa kunitia moyo. nitakaa kimya kwanza ili yeye aanze kwenda mahakamani , nimeshapata mwanasheria ameniambia nisubiri kwanza aanze , halafu hata nyumba tuliyojenga itabidi iuzwe na aanze kutoa matunzo ya watoto. nafikiri atajuta kunianza.
Nashururu sana wana JF wote mlioguswa na tatizo langu.