naomba ushauri wenu

Kama hufanyi makosa unawasi wasi gani.

Huyo anaye kuitwa player ungeomba kamchezo naye basi :violin:

fazaaa hapa tu ndio nimekubaliana na wewe"kama hufanyi makosa unawasiwasi gani?" kijana hebu tueleze kwa ufasaha..nyoosha maneno..
 

umeshawahi kusikia msemo tembea uone mambo? basi ndio hayo sio kila unalosikia ni kweli, watu wanapenda kutia chumvi wanapohadithia maisha na mapirika ya walipo, hawasemi yote na huwezi kuyajua yote hadi pale ukienda mwenyewe na kuona kwa macho yako. Mfano ni huo ulosema kuwa hakuna wakati wa kupoteza kwa ajili ya kazi, sio kweli, mimi binafsi kwa mfano, nafanya kazi jumatatu hadi ijumaa saa tatu hadi kumi na moja na nusu, week end niko off, natumia siku hizo kupumzika, kufanya mambo yangu ya binafsi nyumbani, kwenda kuona mechi za mpira, kutembelea rafiki na jamaa pamoja na kuwasiliana na walio nyumbani. Mara chache huenda ofisini kama kuna jambo muhimu au kama niko nyuma katika moja ya kazi zangu. Sasa tu kwa kuwa wako watu wengine kwa sababu zao wenyewe hutafuta kazi za week end kuongezea na kazi ile ya jumatatu hadi ijumaa, hapo ndio tena wanapowaambia kuwa maisha ya nje hakuna kupumzika au kupoteza muda, lakini ukweli ni kuwa huo ni uamuzi wao na sio hali halisi ilivyo kwa kila mtu. Nadhani umenielewa kidogo.
 

Moja ya mawaidha ninayoyakumbuka kutoka kwa mwalimu mkuu wa skuli tulipokuwa tunaanza primary "tabasamu upate marafiki, utakuwepo hapa shuleni hapa kwa miaka mingi unahitaji kuwa na marafiki, sio kila anaekuchekea anakutaka kimapenzi."
 


Nashukuru kuwa unajua kama ni wake za watu. Ushauri wangu ni kwamba, Ogopa mke wa mtu, usimchezee hata siku moja. Take it from me, mke wa mtu ni hatari mno.
 


Nimekuelewa sana na tukirudi kwenye mada yetu, mambo mawili yanajionyesha hapo. Una wakati wakutembelea jamaa wa kutosha na alhamdullilah una kazi soundly vitu hivi wakati mwengine vinachangia matatizo. Na ndio maana nikasema hapo awali kuwa makini na hizi ulizosema safari za kutembelea jamaa. Hebu jidai kuwa nawe uko bize kidogo ili kupunguza hayo mawasiliano. Wanawake watakutega hao ufikiri kuwa labda wanafatia tabasamu zako kumbe wana hesabu za baadae.
 

Ahsante, nimekuelewa na nitajaribu kufata ushauri wako
 
Mh,mke wa mtu sumu...nafikiri hii ni hatar zaid ya ile inayoingia kwenye born marrow.
 
Mh,mke wa mtu sumu...nafikiri hii ni hatar zaid ya ile inayoingia kwenye born marrow.
 

Sitaki kukutia homa ila nakukumbusha tu simba mwenda kimya ndie mlae nyama. Huyo mumue kuwa anawakalia kimya hao marafiki zako sio kuwa hana nyumba ndogo. infact uliza uambiwe, watu wangapi wamesalitiwa na marafiki zao na wakati wote wakiwa wanaamini kuwa waume zao na marafiki zao hawapatani kabisa?

Wataalamu wa nyumba ndogo ni wajanja na janja moja ni kujifanya anaemngegua hampendi anapokuwa mbele ya wanaowajua. Si unafanya kazi wewe? hujawahi kusikia watu maofisini inapotoka siri yao ya kuwa wana affair na kila mtu kushangaa?

Ukimya na kutoongea na marafiki zako sio dalili ya kuwa hana nyumba ndogo, sio dalili kuwa hamnegui mmoja wa marafiki zako na sio dalili kuwa hammezei mate hata rafiki yako mmoja.

Tabasamu kwa upande wake sio dalili ya kumtaka mtu kabisaaaaa!!!!
 
It's important to understand; personality makes you the way you're.
Ucheshi, uchangamfu, upole zote hizo ni attributes tu, as long as ni tabia poa huna haja ya kujishuku.
Elewa tu kuwa hizo tabia umeumbiwa, kwa kuwa out there, there's some girl who is a perfect fit kuja kumerge na tabia zako.
so patient be you buddy!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…