Nyanidume kama hukuwa na ushauri ungempotezea tu kuliko kutumia maneno makali.Unaonekana wewe una ukabila ndani ya nafs yako ndiyo unaokusumbua, kwangu mi naona ni ujinga kwa msomi kama ww kuumizwa na ukabila, lete jamvin mambo ya mcng na siyo kutuletea habar zako za ukabila hapa.
Kwanza natanguliza shukran zangu kwenu.Nina iman kubwa kwamba nitapata ushauri wa kunijenga kutoka kwenu. Mimi ni kijana niliye hitimu masomo yangu mwaka huu kwa ngazi ya shahada.Katika kipindi chote cha masomo tangu darasa la kwanza mpaka hapa nilipofika,nilikuwa napata support kutoka kwa mama yangu na ndugu wa upande wa mama yangu tu.Najua watu watajiuliza kwanin,ila hili lilisababishwa na kutokuelewana kati ya baba na mama yangu ambako kulipelekea kuvunjika kwa familia.Kwa hiyo kipindi naanza darasa la kwanza niliandikishwa kwa jina la ukoo wa mama yangu ambalo ndio jina ninalitumia mpaka sasa. Sasa tatizo langu liko kwenye jina,mfano unaweza kufika mahali ukajitambulisha kama kama mchaga lakini jina lako la ukoo unalotumia ni la kisukuma,Je hamuoni kama inachanganya watu? Au nibadilishe jina?. kwa hiyo wana jf naomba ushauri wenu uwe specific kwenye jina kwa sababu hayo mambo mengine ya migogoro nimeshayafanyia kazi.
ASANTENI.
Nyanidume kama hukuwa na ushauri ungempotezea tu kuliko kutumia maneno makali.
Kichasi mie nadhani kinachokusumbua si kabila bali unahisi umekosa identity kwa upande wa baba yako. Ili uwe na amani unaweza kwenda kwa Wakili kuandaliwa kiapo (DEED POLL ON CHANGE OF NAME) cha kubadili jina kwa kuongeza jina la ukoo la baba yako mbele ya majina yako ya sasa (hii itasaidia majina yasiwe tofauti sana na unayotumia sasa). Baada ya kusaini hicho kiapo unapeleka kwa Msajili wa Hati kwa ajili ya kusajiliwa na kutangazwa katika Gazeti la Serikali. Hapo utakuwa na majina yanayotambulika kisheria mahali popote. Wengi huapa kisha hawasajili lakini kisheria kuapa kubadili jina bila kusajili ni sawa na zero.
Nakushukuru sana mkuu,kwa ushauri wako uliojaa hekima.