Naomba ushauri wenu kuhusu Chuo cha St. Joseph

Naomba ushauri wenu kuhusu Chuo cha St. Joseph

BABA NEJAD

Member
Joined
Nov 24, 2014
Posts
43
Reaction score
44
Habari za Weekend, natumai muwazima.

Mchana wa leo nimepigiwa simu na mdogo wangu ambae anasoma chuo kikuu cha mtakatifu Joseph kampasi ya Boko katika fani ya Medical Doctor (MD) . Katika maelezo yake alinambia Mkuu wa chuo amewaambia wanafunzi wote ambao wanasoma MD wenye alama D ya chemistry au biology, warudi nyumbani haijalishi wako mwaka wa ngapi kwa sababu wanaharibu sifa ya chuo hicho.

Walipotaka kupewa barua ya kusimamishwa masomo Mkuu wa chuo aligoma, akidai wao wanaangalia cheti tu na hawatatoa barua kwa mtu yeyote bali warudi nyumbani na chuo ndio mwisho.

Kinachoniumiza kichwa ni kuwa huyu jamaa anaingia mwaka wa pili sasa hv, na tangu mwaka jana tumejibana tukalipa ada zaid ya milioni 4 kwa sababu alipewa asilimia 80% ya mkopo kwa hyo kiasi kinachobaki tunamlipia. Vile vile TCU ndio ambao walimdahili na kumpangia chuo hicho na kusajiliwa akaanza masomo tangu mwaka jana, sasa hv wanabadilika kama kinyonga.

Naomba ushauri wenu wadau nifanyaje ili huyu jamaa aweze kuipata haki yake ya elimu au hata kurejeshewa kile ambacho tumelipa kwa mwaka mzima uliopita.

Ahsanteni, natanguliza shukrani zangu kwa ushauri wenu.
 
nimeongea na rais wa chuo hicho bwana Ndimile Kilatu 0756623194 na amesema hakuna kitu kama hicho na hakuna mwanafunzi aliyepewa 80% ya mkopo kwa wanaoingia mwaka wa pili. Kingine ni kwamba bado wako likizo maana walifunga tarehe 28/10/2016 na watafungua tarehe 2/12/2016
 
Hiii habar si ya kweli mm n mmoja wa wanafunzi hapa chuoni. Muulize vizur ndugu yako labda ame discontinue maana hata chuo hatujafungua na raisi wetu Ndimile Kilatu amekanusha hizo taarifa
 
Asante sana kwa kufafanua. Uongo uezidi kusingizia vyuo
 
Hiii habar si ya kweli mm n mmoja wa wanafunzi hapa chuoni. Muulize vizur ndugu yako labda ame discontinue maana hata chuo hatujafungua na raisi wetu Ndimile Kilatu amekanusha hizo taarifa
Nashkuru sana kwa taarifa hii. Nadhani nmepata mwanga sasa wap kwa kuanzia. Pia nashkuru kwa kunipa mawasiliano ya huyu Raisi wa chuo...
 
Hiii habar si ya kweli mm n mmoja wa wanafunzi hapa chuoni. Muulize vizur ndugu yako labda ame discontinue maana hata chuo hatujafungua na raisi wetu Ndimile Kilatu amekanusha hizo taarifa
Upo sahihi Mkuu. Nlikua npo barabarani so nkashindwa kureply. Nmembananisha hp anadai wako 15 wameandikiwa disco lakin masomo aliyofaulu yamepita ufaulu, akapeleka taarifa kwa Dean ndo akamwambia wameamua kuondoa wote wenye D makusudi kwa sababu wanaharibu sifa ya chuo yeye ni mmoja wapo. Wacha nizungumze na huyu Rais anithibitishie kabla sijachukua hatua zaid. Zaid ya yote nashkuru sana kwa taarifa zenu wote. Bila ya nyinyi nadhani nngekua na mawazo negative ya hiki chuo. Nashkuru sn kwa kunifungua wadau.
 
Huyo atakua kadisco mana haiwezekan wahind wazibue sheria zao fasta mie nimeshangaa
 
Ha haaaa ...dogo kadisco halafu analeta usingizi .JF imemuumbua
 
Back
Top Bottom