habari zenu wana jamvi,leo nimekuja hapa kwa minajili ya kupata ushauri wenu,mi ni kijana wa miaka 22 lakini mungu amenijalia nimepata ajira ya kudumu serikalini na yenye maslai mazuri,kwa sasa nimeanza kujitegemea na sina mpango wa kuoa 7bu nina mpango wa kuoa nikiwa na miaka 25 au zaidi.daima cjawa tayari kuwa kwenye mahusiano na mpaka sasa nipo cngo.
linapokuja swala la kuoa naona kama naanza kutafuta maisha upya jinsi swala hili ninavyo liona zito,wengi wananishauri n vyema kuwa na mchumba mapema ili kujuana tabia lakini point ya age difference ndo imekuwa tatizo maana wengi wanasema age difference ifike miaka 5 na kuendelea,kwa maesabu hayo kwa harakaharaka natakiwa nikatafute mtoto wa form 3 or 4.kitu ambacho czani kama kimekaa sawa,kwa kutambua kuwa humu ndani mpo watu wenye umri sawa na wazazi wangu najua mtanipa ushauri ambao either uta boresha ule tunaopatiana vijana mitaani au kubadirisha kabisa.
NAWASILISHA