naomba ushauri wanajamii forum

naomba ushauri wanajamii forum

mwita mohere

Member
Joined
Mar 15, 2013
Posts
23
Reaction score
1
katka maisha kila mtu ana mikasa na historia zke mimi ni mwanachuo mwaka tatu chuo cha ifm nasomea bachelor banking and finance hata hivo tatzo langu ni hiv nkigraduate july2013 cna mahala pa kikaa hapa mjin nkifanya mipanho yaa mishe itanbidi niende kijijin ambako hata mitandao ya neti hamna kabisa nimezhindwa nfanyeje maana kma mnvyojua mishe zote hasa za kibenki znfanyiwa huku mjin(dar)ebu nshauri ntumie njia gan kusolve tatizo langu
 
katka maisha kila mtu ana mikasa na historia zke mimi ni mwanachuo mwaka tatu chuo cha ifm nasomea bachelor banking and finance hata hivo tatzo langu ni hiv nkigraduate july2013 cna mahala pa kikaa hapa mjin nkifanya mipanho yaa mishe itanbidi niende kijijin ambako hata mitandao ya neti hamna kabisa nimezhindwa nfanyeje maana kma mnvyojua mishe zote hasa za kibenki znfanyiwa huku mjin(dar)ebu nshauri ntumie njia gan kusolve tatizo langu
Si kweli. Unless uniambie huo mkoa ambao hutoweza kufanya applications.
Good news siku hizi kuna internet hadi vijijini. Pia ofisi za posta zipo karibia kila wilaya.
Magazeti pia yanafika ingawa kuna delay ya one day kwa mikoa mingi but but ni muda mwafaka.
Hebu niambie ni mkoa gani huo utakao enda baada ya kumaliza masomo ambapo hauna interent, maagazeti hayafiki, simu hazipatikani, hakuna ofisi za posta. n.k.
 
Vijana wengi wanatembea na cv zao mda mrefuu kwa sababu kama izo za kung'ang'ania kubaki dar baada ya chuo.. kama huna ndugu au jamaa wa karibu dar tafuta mkoa mwingine utakaopata msaada..
 
NMB yupo kila sehemu,, na CRDB nae anajitahidi,,, au unataka bank za mliman city na quality centre ili ukitoka kazini jion uende savanah?

Maisha popote kijana
 
tafuta hela kidogo tuchange tuchukue chumba dar wakati tunafuatilia hizo mishe za kazi.
 
Nenda kapangishe room mitaa ya survey.
 
nenda kijijini tu hapa mjini utasanda uone maisha magumu, uishie kujinyonga maana wana chuo hamnaga uvumilivu
 
Mmh! hata mgumu magazeti ya leo kesho saa nne asbh unayapata, acha woga cha msingi ni kumuomba Mungu tu ndiye atoae riziki, unaweza baki dar na bado usifanikiwe
mkoa ni mara lakin kijini xna
 
nakushauri jiunge na huduma za maktaba, ambapo kwa mwaka ada ni 10000 tu kuwa member,ivo itakuwa ni rahisi kujipanga hata kwa wiki kwenda mara moja library ya mkoani kwako kusoma magazeti bure, mfano magazeti ya daily news,gurdian na mengineyo ambayo huwa na nafasi za kazi huwa yanapatikana library yoyote ile ya serikali, pia ukiwa member wa library huduma za internet huwa zinatolewa kwa bei nafuu sana, na pia library nyingi za serikali cku hizi huwa na internet, so unaweza rudi mkoani kwako na ukaendelea na application zako cha msingi jitahidi uwe unajikusanya ili zinapotokea interview uwe na uwezo wa ku attend,wengine tumejaribu kufanya hivyo imetusaidia kiasi fulani, lakin dar kama huna source of income kwa kweli itakugharimu sana kwa sababu pia hujui ni lini utapata kazi mana kuapply kazi sio kupata mana wasomi ni wengi.
 
Watu wanakubeza hapa lakini naamini unachosema na kina ukweli kwa asilimia nyingi kazi yako unayotaka ni rahisi kuipata au hata kuhudhuria intavyuu ukiwa mjini.
Cha kufanya

1. Wakenya wengi wakimaliza chuo hasa nairobi huendelea kukaa hostel hata miaka miwili zaidi mpaka mambo yanapokuwa sawa hasa kutokana na urahisi wamaisha ya hostel. Pia nilikutana na jamaa fulani wa ki-nigeria huko lagos katika kufauatilia ingawa jamaa alikuwa anafanya katika inter. org alikuwa bado anaishi chuoni japo alikuwa na mwaka baada ya kumaliza chuo...Nakushauri uendelee kukaa hapo hostel either kwa kubebwa na rafiki wa darasa la chini au utafute mwenzio mwenye uhitaji kama wako mpange chumba/hostel cha bei rahisi muendelee kutafuta maisha.

2. Tafuta kazi ya namna yeyote sio lazima ya ulichosomea kwa sasa ili upate kipato japo kitakuwa kidogo cha kukuwezesha kuendelea kukaa mjini kama nauli chakula, pango la ghetto n.k. Kazi hizi ni kama kwenye saccoss na micro-finance, data entry kama airtel/tigo n.k, kuwa commision agent kwenye ofisi za kampuni za simu, waiter katika hoteli na restaurant kubwa mjini etc

3. Fanya biashara ndogo ndogo wakati unatafuta kazi au wakati unajiandaa kufanya biashara kubwa. Kwa mfano kuna jamaa flani alimaliza chuo akawa hana kazi, jamaa akawa anaishi na mjomba yake maeneo ya dar ambaye nae ni hohehahe basi jamaa akawa anafanya biashara ya kuuza saa (watch) na mikanda (belt) huko posta. Mtafutaji huyu akwa hakosi hata TZS 10K kama faida kwa siku. Basi tatizo likawa akionana na wenzie aliosoma nao ambao walipata kazi katika maofisi makubwa kubwa posta jamaa akawa anaona aibu lakini hakuwa na jinsi akendelea hivyo hivyo. Baada ya muda akapata bonge la kazi katika taaasisi fulani nyeti hivi sasa mambo yake mazuri.

4. Mwisho - huko kijijini wanaamini wewe uliosoma ndio mjanja, sasa ikiwa na wewe utamaliza na kwenda kukaa unakuwa unawakatisha tamaa baadhi ya wazazi wenye kasumba ya kuwaambia wanao hasa linapokuja suala la ada kuwa kusoma hakuna maana, fulani amesoma huko dar mpaka chuo kikuu lakini amerudi tupo nae hapa. Hivyo kama huna plan za maana kama kulima, kufundisha, kuanzisha mradi huko kijijini ni bora ugangamale hapo mjini....

5. Mtafutaji hachoki- akichoka kapata....zaidi siku nyingine....
 
wehoodie nakushukuru sana maana hayo mawazo ulionip ni muhimu sana naamin yatansadia
 
Back
Top Bottom