Naomba ushauri wa mawazo wakuu!

Naomba ushauri wa mawazo wakuu!

Perry

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
10,082
Reaction score
2,358
Wakuu,my Ex girlfriend alifariki kwa ajali ya gari cku chache zlizopita huko jijin darslam,asa ndugu zake katika kupanga panga vitu vyake kwenye kabati,wakakutana na notebook ambayo huyo my ex alipenda kuandika kumbukumbu za matukio yake muhmu,na katika kuichunguza hyo notebook wakakuta mahali ameandika namna alvokutana na mimi,na jinc alvokua ananipenda na kunichukulia kama mpenzi na rafiki wa maisha yake na kuna mahali ameandka kwamba,ingawa mie na yeye 2mekwisha achana kwa sababu ambazo yeye amesema kwamba mimi nlikua msaliti kwake,lakini ataendelea kunipenda na kunithamin mpaka cku kifo kitakapo mwondoa duniani..sasa shangazi yake kanitafuta kwa kutumia number ya huyo Ex,ameniambia nifike nyumbani kwao angalau wanijue...sasa wakuu,nauliza kuna umuhmu wa mimi kwenda huko kwao kweli au ntakua naenda kujichoresha tu?
 
Sio jambo baya kwenda kwao nadhani pia ni jambo litakalodhihirisha kuwa ulimpenda. ikiwa una hakika hakuna jambo baya ulilowahi kumfanyia na mliachana kistaarabu huna haja ya kutoenda. ni vema ukimuenzi hata kwa kwenda kuweka shada la maua kwenye kabuli lake.
 
Mkuu Perry, pole kwa msiba,

Sidhani kama ni jambo rahisi kumtoa mtu mkoa mwingine aje mfahamiane tu, simply kwa maandishi ya notebook/diary! Labda maelezo hayo yaliambatana na kutaka kukupa taarifa za msiba. All in all, Ni vizuri kufika huko katika msiba (hata kama si kwenda kuitikia wito bado ni vyema kuhani) maana kiasi fulani mlikuwa/mliwahi kuwa na mahusiano ya karibu.

Hata hivyo, ni bora kupeana taarifa na "girlfriend" au mke uliyenae (kama yupo), pili jiandae kwa lolote (gharama za kifedha zaidi) maana waelekea kwenye shida/msiba na si sherehe...Mwisho pole tena kwa msiba.
 
Last edited by a moderator:
kwa hiyo Shangazi alivopiga sim ndio alikueleza hayo maneno yote ktk diary

Kama una nafasi nenda....ingekuwa alijinyonga labda na kuacha hako kaujumbe yangekua mengine
 
Nenda mwana, si unajua ndugu wantaka wajifariji kupitia wew hasa katika hiki kigumu au hutaki kumuenzi? kama alivyokuenzi kwenye dairy?
 
Wakuu,my Ex girlfriend alifariki kwa ajali ya gari cku chache zlizopita huko jijin darslam,asa ndugu zake katika kupanga panga vitu vyake kwenye kabati,wakakutana na notebook ambayo huyo my ex alipenda kuandika kumbukumbu za matukio yake muhmu,na katika kuichunguza hyo notebook wakakuta mahali ameandika namna alvokutana na mimi,na jinc alvokua ananipenda na kunichukulia kama mpenzi na rafiki wa maisha yake na kuna mahali ameandka kwamba,ingawa mie na yeye 2mekwisha achana kwa sababu ambazo yeye amesema kwamba mimi nlikua msaliti kwake,lakini ataendelea kunipenda na kunithamin mpaka cku kifo kitakapo mwondoa duniani..sasa shangazi yake kanitafuta kwa kutumia number ya huyo Ex,ameniambia nifike nyumbani kwao angalau wanijue...sasa wakuu,nauliza kuna umuhmu wa mimi kwenda huko kwao kweli au ntakua naenda kujichoresha tu?
Busara inahitajika hapo..sio kukurupuka!
 
Back
Top Bottom