Naomba ushauri wa kisheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba ushauri wa kisheria

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Fblukuwi, Aug 10, 2011.

 1. F

  Fblukuwi Senior Member

  #1
  Aug 10, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wanajamii naomba ushauri wenu wa kisheria.
  Sisi wafanyakazi wa Hospitali ya mji wa NJOMBE iitwayo KIBENA tulihamishwa kuanzia Juni 2010 kutoka kwa mwajiri wetu wa awali ambaye ni DED - NJOMBE DC tukapelekwa kuwa chini ya TED-NJOMBE TC ingawa kituo chetu cha kazi kilibaki kuwa Kibena Hospitali lakini tulipata usumbufu wa mafaili yetu kuhamishwa kutoka ofisi moja hadi nyingine ambapo baadhi yetu mishahara ilimix up na wakachelewa sana kulipwa pia hata kazi za malipo ya ziada yalicheleweshwa sana.
  Kwa kawaida mfanyakazi anapohamishwa huwa anastahili malipo mbalimbali kama subsistency allowance, distrubance allowance pia travel allowance. Tulipoulizia kwa mwajiri wetu mpya NJOMBE TC alijibu kuwa hatustahili chochote. Je mwajiri wetu yupo sahihi au katupiga changa la macho?
   
 2. E

  Edison JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 487
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  kuna utaratibu unaodai kwamba wanaangalia distance below 8km hulipwi hata senti tano! ila wanadai kama kuna usumbufu wa hapa na pale basi mwajiri atatumia busara zake kuona kama mtumishi anastahili kulipwa au la?
   
 3. m

  mnozya JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma na kanuni zake za mwaka 2003 hakuna malipo mnayotakiwa kulipwa.

  Aidha kwa mujibu wa sheria ya mahusiano kazini namba 6 ya mwaka 2004 (ambayo kwa sasa ndiyo sheria inayotawala mahusiano yenu na mwajiri wenu mpya) hampaswi kulipwa hayo malipo.

  USHAURI
  Kaeni na mwajiri wenu muombeni tu atumie hekima na busara kama ataweza ILA hawajibiki kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria
   
Loading...