Usharekebisha mapungufu yaliyojitokeza ambayo yalisababisha ukaachana na mwenzi wako?
Haina maana umeachana na mtu leo kutokana na mapungufu yako kesho upo na mahusiano mengine na bado unarudia tabia zilezile.
Pia mkuu, ukiachana na mtu unajipa muda kuona kama kweli maamuzi uliyofanya yalikua sahihi au ni mihemuko tu.
Mfano: Wewe umeingia kwenye mahusiano mapya baada ya kuachana, lakini mwenzi wako akatulia na baadaye akaingia kwenye mahusiano yake, wewe ukajikuta unamuonea wivu bado (bado unampenda), hii itakuathiri kisaikolojia.