mi nipo dom, kama uko vzr tuanzishe wedding planer na fashion. Kitu hii inalipa na dom hakuna!Nataka kufanya biasha na mtaji ni dola 8500 lakini mpaka sasa sijajua nifanye biashara gani naombeni ushauri
Next time kabla ya kuwa na hela unatakiwa uwe na wazo la biashara itakusaidia zaidi maana hata hiyo dola 8500 uliyonayo ungeweza kuitumia nusu lakini ukija hapa na amount kila mtu atakuwa anakupa biashara zinazo-range hiyo amount kumbe kuna biashara zingine nzuri zaidi ambazo ungezifanya kwa hela chini ya hapo, xfactor amekushauri uende jukwaa la biashara huenda ukapata kitu pia tujenge tabia ya kuwa na mawazo ya kibiashara katika kipindi ambacho hatuna kitu hata siku utakapopata pesa unaleta idea zako angalau mbili au tatu alafu watu tunakusaidia kuzi-refine mwisho wa siku unatoka na kitu kizuri
Huo ni ukweli mtu mkuu yaani ukiwa unafanya kitu chochote, wakati upo katika kipindi kigumu wewe ndio unaweka miundo mbinu sawa, hata kama unajenga design na marekebisho mbalimbali unakuwa nayo in advance pia unafanya consultation hivyo ukipata ela tu unafanya kweliThis is very true.umenikumbusha rafiki yangu mmoja wa siku nyingi,yeye alikuwa anafanya research ya biashara ya kufanya wakati tulikuwa tunajua hana hela,so tulivyo ona anafanya research tukajua mwenzetu kapata bingo ila yeye akatuambia kuwa hana hela ila anajiandaa siku akipata hela hatokosa cha kuifanyia hiyo hela.usisubiri upate hela ndio utafute idea,anza sasa kufanya uchunguzi kujua hasara na faida ili ukipata hela ibaki kutekeleza tu