Naomba ushauri wa biashara!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba ushauri wa biashara!!!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Pindima, Nov 14, 2011.

 1. Pindima

  Pindima JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 349
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wana jamii wenzangu naomba msaada wa mawazo!!Nna million 50 na nataka kufanya biashara ila mpaka sasa sijui nifanye biashara ipi?!!naombeni msaada wenu tafadhali!!
   
 2. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  naona mkuu thread yako umeiweka kwenye jukwaa la malalamiko, wasiliana na MODS waipeleke jukwaa la Biashara
   
 3. Pindima

  Pindima JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 349
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Poa asante ndugu!!bado mgeni kwenye hii JM mambo mengine yanasumbua!!
   
 4. j

  josepher Member

  #4
  Nov 16, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Nakupongeza kwa kuwa na mtazamo mkubwa wa kufanya biashara,nipatie number yako niweze kukusaidia kiushauri,nafanya training pia consultation kama mtu anahitaji kufanya biashara gani afanye,pia naweza kukuunganisha na wafanya bishara wakubwa wa kimataifa,mimi napatikana kwa 0656020703/0786020703
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu

  mimi nadhani ungeeleza unanuia kufanya biashara gani ambayo kwa uelewa wako unaona itakuletea faida either unaweza kugusia sector za kibiashara unazoona zinafaida kama food & beverage, transportation, agriculture, poultry, construction, retail, entertainment etc

  nadhani hapo utapata mawazo na ushauri wa kina na utafaidika
   
 6. M-pesa

  M-pesa JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kuwa makini na hizi consultation za kukutana na mtu usiyemfahamu. Utapukutishwa 50 Mn yote! Na utaishia kutupa history kuwa uliwahi kumiliki milion 50.
  Anza kwa kutupatia SWOT analysis yako, then tutakupa ushauri.
   
 7. babalao

  babalao Forum Spammer

  #7
  Nov 16, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hiyo milioni 50 umepataje? nakushauri utumie mbinu hizo hizo ulizozitumia kupata milioni 50 kupata zingine. Ukiwa na maswali nipigie simu 0755394701 naweza kukupa ushauri wa biashara gani ufanye, kwani lazima tukague vipaji vyako kujua unaweza kufanya biashara gani. Mimi ninatoa ushauri wa biashara, mafunzo ya ujasiriamali na kuandaa michanganuo. Pia ni mtunzi wa kitabu cha Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri
   
 8. Erick_Otieno

  Erick_Otieno JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 28, 2010
  Messages: 630
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 180
  Fanya biashara unayoipenda yaani iliyo ndoto yako. Jifunze toka kwa watu ambao wanaoifanya hiyo biashara na utapata somo zuri tu na mafanikio safi. All the best
   
 9. matron

  matron Member

  #9
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 13
  hata ukipata business partner hakikisha hajui una mtaji kiasi gani maana kikulacho ki nguoni mwako,kuna jamaa yangu alidunduliza kamtaji kake akashauriwa na rafikiye wakafanye biashara za kupitisha sukari tokea zanzibar (magendo) walianza vizuri trip ya kwanza ile wanarudi mara ya pili rafiki akamlengesha kwa mapolisi na kutoa data zote..kilichofuatia ni kukamatwa ovyo na kutoa rushwa na mwisho mmoja wa askari akamwambia anayekumaliza ni huyo mwenzako,so watch out na hawa wanaokuita .nyie kama mnataka kumshauri kwanini msiweke hapa kama wenzenu mfano malila na kina Lat ?
   
 10. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,128
  Trophy Points: 280
  Mkuu aidia nzuri zitatoka kwako wewe mwenyewe, ni vigumu sana kupata kile unacho taka wewe, jalibu kukaa chini na not book na kutengeneza aidia nying sana theni zichuje zibaki kama tano hivi theni sasa zilete huku ili wakuu wakupe maoni yao,so fanya hivyo list aidia zako theni zichuje zibaki chache theni leta humu janvini
   
 11. Pindima

  Pindima JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2011
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 349
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Asante kwa ushauti naweza sema ni mzuri kw wote waliochangia!!mawazo yenu yamenifanya nikae tena chini na kufikiria la kufanya!!
   
 12. Pindima

  Pindima JF-Expert Member

  #12
  Nov 18, 2011
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 349
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Asante kwa ushauri naweza sema ni mzuri kwa wote waliochangia!!mawazo yenu yamenifanya nikae tena chini na kufikiria la kufanya!!
   
 13. s

  sanjo JF-Expert Member

  #13
  Nov 18, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mkuu,

  Biashara ni kazi kama kazi nyingine ya kawaida. Hivyo, biashara ina misingi na miiko yake.

  Misingi ya biashara.
  (1) Penda biashara yako
  (2) Mteja wa biashara ni nguzo muhimu sana.
  (3) Bidhaa au huduma itowayo lazima iwe ni kukidhi mahitaji wa wateja wako. La sivyo, hao wateja hawana sababu ya kununua hizo bidhaa zako au huduma zako.
  (4) Hifadhi mtaji wako (Preserve your business seed capital). Biashara inahitaji mtaji katika shughuli zake za kila siku (working capital) na katika kufanya upanuzi wa shughuli zake (capital expenditure).
  (5) Mtaji watu na usimamizi (human capital & management). Biashara huuendeshwa na watu hivyo ni muhimu kuwa na watu weledi na wachapa kazi wenye uwezo wa kuelewa biashara, wateja na mwelekeo (future trends). Usimamizi wa biashara ni muhimu sana. Bila ya usimamizi hata kama una mtaji mkubwa na wateja wengi biashara hiyo haitadumu.
  (6) Sheria za kiabiashara (Regulatory aspect of doing business). Biashara nyingi zinaendeshwa kwa kuzingatia sheria na taratibu mbalimbali. Muhimu kuzielewa na kuzingatia sheria na taratibu hizo ili kuepuka kuzivunza taratibu hizo. Hapa vile vile angalia muundo wa biashara yako, yaani kama ni sole proprietorship, limited liability company au partnership.

  Miiko ya biashara:

  (1) Usile mtaji
  (2) Kumdharau mteja. Mteja ni mfalme/malkia biashara ifanywayo bila kuzingatia matakwa ya wateja haiwezi kudumu.
  (3) Kuridhika. Biashara hubadilikabadilika kila wakati. Hivyo, ubunifu wa kutaka kuendelea mbele daima ni muhimu sana kutokana na ushindani.

  Hivyo, kwa kuwa una TZS50.00m mkononi zingatia hayo. Kaa chini jiulize biashara ipi unaipenda sana, Uko wapi (location), bidhaa yako utaitoa wapi? utaifarishaje? je ina wateja wengi? upi ni mwelekeo wake (its future outlook)?, je unawashirika wazuri? Vipi huduma za kibenki? etc
   
 14. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #14
  Nov 18, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  sanjo heshima yako mkuu,
  hata mie kadawa kako kamenitibu,we ni jembe ni lazima upewe pongezi zako tunaitaji mavituzi na nondo kama iz bwana
  thax
   
 15. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #15
  Nov 18, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mmh, siusemei moyo lakini mkuu, mwenye mtaji wa 50m sio level ya clients wako, kama una contacts na wafanyabiashara wakubwa duniani. Au huzungumzii kina warren buffet nk?
  I'm just thinking.
   
 16. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #16
  Nov 18, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mkuu kama huna experiance ya biashara na hujui nini ufanye na 50 zako, ni too risky kuinject hiyo pesa kama muanzaji. Nakushauri utakapopata idea ya nini cha kufanya anza taratibu na mtaji mdogo kidogo ya huo, kama 10-15m kwa kuanzia, hii itakusaidia kuwa na back up ya kutosha kukabiliana na contingencies za kibiashara. Jipe muda wa kugrow taratibu, ndani ya mwaka utakuwa na uzoefu wa kutosha na utakuwa umeshajifunza mengi sana.

  Siri kubwa ya biashara si idadi ya pesa mingi utakazoingiza kama mtaji au katika mzunguko. Siri ni kuwa na muda wa kutosha kusimamia biashara yako, kujifunza zaidi na zaidi kila siku. Na kujituma pamoja na kujifunza kutoka kwa wengine...

  Kama utasisitiza kuanza na 50m, Binafsi ningekushauri ununue tractor unit moja na trailer yake kutoka UK, wakati ipo njiani anza mchakato wa kukuza mtandao wako na wafanya biashara hiyo. Utajifunza mengi ndani ya mwezi na utakuwa tayari kuifanya gari itakapofika. Ukiwa na bima salama, na dereva mwerevu na mweledi, ndani ya mwaka utakuwa umesharudisha hela yako. Na unaweza ukawa na mawili ndani ya miezi 10, hii ni pale tu utakapokuwa na adabu na fedha (usifanye matumizi holela ya mapato yanayotokana na gari). Na kama uko tayari, safiri nalo gari lako. Anza na mbao mafinga to dar, trip 1 ni 2.5m, kwa mwezi unaweza kupiga hizi kama 7 kama uko serious.

  Karibu.
   
 17. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #17
  Nov 18, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  naona watu mnazimendea fedha za jamaa zaidi ya fisi na mifupa,namba za simu kibaoooo!!lol,ushauri wako kuwa macho,humu jf wezi kibao
   
Loading...