NAOMBA USHAURI WA BIASHARA YA UWAKALA M PESA

NAOMBA USHAURI WA BIASHARA YA UWAKALA M PESA

mwampepe

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2015
Posts
331
Reaction score
130
Habari, Sorry,nahitaji kuanzisha biashara ya uwakala wa fedha eg. Mpesa,halopesa n.k naomba ushauri nifanye nini ili nipate faida kubwa,changamoto zake ni zipi? Nifanye nini ili niwe salama Mimi pamoja na pesa zangu, naomba ushauri kwa yote ambayo siyajui kuhusiana na uwakala please

Thanks in advance
 
achaa iyo biashara ni kama una wafanyia watu wa mitandao ya simu na bank kwa mwezi una weza pata gawio 19k kabla ya makato ya kodi
 
Kwanza kabisa, ushauri wangu ni huu:

1. Mtaji: Anza na mtaji unaoweza kuumudu. Hakikisha una float na cash ya kutosha ili usikwame kuhudumia wateja.
2. Eneo: Chagua sehemu yenye watu wengi, karibu na soko, standi au maduka.
3. Mitandao: Sajili mitandao zaidi ya mmoja kama M-Pesa, HaloPesa, Airtel Money na Tigo Pesa ili kuongeza wateja.
4. Usalama: Usitoe pesa kabla ya kuthibitisha muamala kwenye mfumo wako. Usimpe mtu PIN au simu yako ya uwakala.
5. Faida: Andika kila muamala, hesabu faida na matumizi kila siku. Usichanganye pesa ya biashara na matumizi binafsi.
6. Changamoto: Wizi, utapeli wa SMS feki, kukosa float, ushindani na faida ndogo kwa kila muamala.

Ushauri wangu mkubwa: Usikimbilie kufungua uwakala kwa sababu ya kuona wengine wanafaidika. Kwanza fanya utafiti wa eneo, hesabu idadi ya mawakala waliopo na makadirio ya wateja kwa siku.

Pia hakikisha unasajiliwa kupitia kampuni au msambazaji rasmi na unaelewa masharti ya uwakala kabla ya kuanza.

Kumbuka, uwakala ni biashara ya mzunguko wa fedha; siri ya mafanikio ni usimamizi mzuri, uaminifu na usalama wa mtaji.
 
Habari, Sorry,nahitaji kuanzisha biashara ya uwakala wa fedha eg. Mpesa,halopesa n.k naomba ushauri nifanye nini ili nipate faida kubwa,changamoto zake ni zipi? Nifanye nini ili niwe salama Mimi pamoja na pesa zangu, naomba ushauri kwa yote ambayo siyajui kuhusiana na uwakala please

Thanks in advance
Umakini unahitajika sana kwenye hiyo biashara ,ukifanya uzembe tu UNAACHA NDALA.

Either kwa kupigwa na matapeli au Majambawazi.
 
Habari, Sorry,nahitaji kuanzisha biashara ya uwakala wa fedha eg. Mpesa,halopesa n.k naomba ushauri nifanye nini ili nipate faida kubwa,changamoto zake ni zipi? Nifanye nini ili niwe salama Mimi pamoja na pesa zangu, naomba ushauri kwa yote ambayo siyajui kuhusiana na uwakala please

Thanks in advance
Kupanga ni kuchagua. Kila la heri kwako
 
achaa iyo biashara ni kama una wafanyia watu wa mitandao ya simu na bank kwa mwezi una weza pata gawio 19k kabla ya makato ya kodi
Sijui utakua mzembe kiasi gani hadi upate 19k kwa mwezi mzima hiyo si hela ya siku tatu hadi nne tu
 
Kama pesa yako ni kubwa mkuu go for other issues inapilipili nyingi sana but kama umeona unaweza kuifanya kwa moyo then go for it
 
Mengi yameshaongelewa, mi najazis tu,
Kwenye hiyo biashara unatakiwa uwe na akili timamu, hakikisha hauchanganyi hela ya biashara na matumizi yako BINAFSI.

Matapeli wananjia nyingi, hivyo basi kua makini, na ni maruku kupokea simu ya uwakala ukiisia inaita.

Mwisho, uwe na Lipa namba, hii itakusaidia kupata faida ya hapo hapo kwa kila muamala (hapa ndo unaweza ukachomoa hela ya kula)
 
Niliunganisha hii biashara kwenye duka langu aisee sitaki hata kuskia, wafanyakazi hata uwape mbinu zote kuepuka utapeli haipiti miezi mitatu wanapigwa parefu, kuna kipindi walipigwa mpaka ukiona simu ya mfanyakazi unajua kishanuka huko... nikasema ya nini
 
Kwa kifupi hii biashara adui zako wakubwa wawili ni 1) matapeli- hawa wanatumia ujanja ujanja na sound nyingi kuchukua vya kwako
2) majambazi- kama sehemu haina usalama vizuri na wakishajua kua una uwezo wa kufanya miamala mikubwa usishangae siku wakaja kukusaidia kufunga hesabu
 
Back
Top Bottom