Naomba ushauri, nataka kununua Toyota Rush

Naomba ushauri, nataka kununua Toyota Rush

upeo

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2013
Posts
369
Reaction score
222
Wakuu nimerudi tena naomba ushauri kuhusu Toyota Rush. Niliwahi kuandika kuwa ni nataka kunua rush, lakini mambo yalikuwa hayajakaa vizuri nikaahirisha lakini sasa hivi nipo tayari.

Najua Toyota ni gari nzuri lakini kuna engine tofauti tofauti na pia watu wengi utawasikia nunua gari toleo la mwaka fulani usinue toleo la mwaka fulani, na pia utawasikia watu wanasema nunua rush yenge engine fulani na ya mwaka fulani.

Swali langu; je ninunue rush toleo gani ni yenye engine gani nzuri?

Nashukuru.
 
Hivi Toyota rush mnavipendea nini? Fuel consumption? Ama nini? Kuna gari ambazo bei ipo juu lakini ni vigari hovyo sana, ni raisi hata kubebwa na upepo, kina shape kama visuzuki vile wanavyopenda wachaga.
 
Kimeo hicho
Screenshot_20210117-190605_Chrome.jpg
 
Kuna gari inaitwa prius utafurahi mwenyewe

Yani nipo kwenye mchakato haitofika may nitakuwa nayo,nipe uzoefu kama unayo maana nimeifatilia sana nimeona mafuta inanusa coz ni hybrid
 
Ninaamini unazungumzia Rush toleo la kwanza j200 na j210. Hii gari nimetumia kwa muda sasa zina engine mbili tofauti k3 (1300 cc) na 3sz-fe 1500cc. Binafsi nakushauri uchukue 3sz kwaajili ya nguvu.
Changamoto kubwa ya hii gari ni mafundi. Hii gari ni daihastu, mafundi wengi zinawazingua hasa kwenye umeme, hivyo kuwa makini kwa fundi unayempelekea. Mfano unaweza kwenda service fundi akakushauri badili plug, ukaweka ngk etc.. gari litapiga miss mpaka unaweza badili fuel pump, kumbe hii gari inafanya poa na plug za denso japo ndo bei rahisi.

Kingine spare zake kidogo zipo bei juu, ukilinganisha na magari mengine ya Toyota. Ila kama utalitunza ni gari umbalo unaweza kumaliza hata mwaka hujaenda gereji zaidi ya kubadili oil. Kwa kifupi changamoto kubwa za hii gari ni zakujitakia mwenyewe, unagusa A unapata B,C,D..

Faida kubwa ni gari ipo juu, unapita karibia kila mahali bila kugonga chini, pia inafanya ujiamini zaidi kwenye safari ndefu. Faida nyingine ni ulaji wa mafuta, kwenye hili ipo poa sana ukilinganisha na size yake. Mfano mafuta ya 120k unatoka dar mpaka moshi na mafuta yanabaki tena ukiwa na abiria.

Kwa kifupi ni gari nzuri nakushauri uchukue.
 
Back
Top Bottom