Naomba ushauri; muda wa kupata mke umefika

Jan 15, 2015
11
3
Naitwa Ahmady niko Dsm, mwaka jana nikiwa field nilitokea kumpenda msichana ambae nae alionesha dhahiri kwamba ana mapenzi ya dhati kwangu kwani vitu vingi alinifanyia kwa muda mchache ambao nilikuwa nae.

Ila mimi nilikuwa na mpenzi wangu ambae tupo yapata miaka miwili tena mtoto nimezaa nae but muda umefika wa kuchagua mke wa kuoa naomba mnishauri wapi niende kati yao ?
 
Unataka tukuchagulie ili akikusumbua uje kulialia hapa JF , haya mkuu mi nakushauri tafuta wengine wawili kwanza tukuchagulie vizuri, multiple choice ya a na b hainogi, wajaze kuwe na a , b , c , d

Halafu usisahu na picha tafadhali
 
vitu gani vingi alivyokufanyia huyo mpenzi mpya kwa muda mchache tutofautishe na huyo wa awali uliyekwisha zaa nae?
 
huyo msichana uliekutana nae field, huenda ana mtu anaempenda sana kuliko wewe, na wameshawekeana hata ahadi ya kuoana, na huenda kashamzalia mtoto, ila yote hayo huwezi ukayajua. ila amekutana na wewe tu huko field kwa muda mfupi kama ajali..
Jiulize kwanini unasita kumuoa moja kwa moja na kumuacha mpenzi wako aliyekuzalia hadi mtoto, na ni kipi kilichokusukuma hadi uje na uzi wa kuomba ushauri!
 
Dini yako inaruhusu oa wote na IKITOKEA UKAMPENDA MWINGINE WA HUMU JF (MAANA NAE ATAKUONYESHA MEMA KWA MUDA MFUPI LAZIMA UDATE) CHUKUA TU.
 
Naitwa Ahmady niko Dsm, mwaka jana nikiwa field nilitokea kumpenda msichana ambae nae alionesha dhahiri kwamba ana mapenzi ya dhati kwangu kwani vitu vingi alinifanyia kwa muda mchache ambao nilikuwa nae.

Ila mimi nilikuwa na mpenzi wangu ambae tupo yapata miaka miwili tena mtoto nimezaa nae but muda umefika wa kuchagua mke wa kuoa naomba mnishauri wapi niende kati yao ?
Ungechagua kabla ya kuzaa.... Huyo uliyezaa naye umwachie nani?
 
Back
Top Bottom