Naomba ushauri kuhusu hii iPhone

moghasa

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
1,084
Reaction score
1,254
Nina iphone ambayo to be honest niliiokota bank huku mkoa sasa imezima, haiwaki!! vp wakuu ndo imekuwa toy au kuna namna ya ku unlock??
 
Nina iphone ambayo to be honest niliiokota bank huku mkoa sasa imezima, haiwaki!! vp wakuu ndo imekuwa toy au kuna namna ya ku unlock??

Maelezo yako hayajitoshelezi kusaidiwa
 
Ukiokota kitu chochote si mali yako peleka police. Hiyo simu kama imeunganishwa na icloud utakamatwa siku yoyote
 
Nitakuwa sijakosea kukuita wewe ni mwizi kama wezi wengine......kwa kuwa kitu ulikiokota na ukauchuna kwa kudhani umelamba dume.....inawezekana ulimuona aliyeiangusha isipokuwa kwa tama zako ukauchuna huku ukimcheki jamaa akihangaika nkuitafuta simu yake bila mafanikio.....

ulikuwa unamcheki kwa jicho la kebehi kwani unajua kuwa simu unayo wewe isipokuwa kwa makusudi kabisa ukaamua kuuchuna......au pengine ulikuwa miongoni mwa waliopigwa na mshangao baada ya kusikia kuwa simu imepotea huku ukionyesha sura ya huruma kwa kujifanya umesikitishwa na tukio hilo ili hali ni mnafiki......

Bado hujachelewa......usingoje hadi ukamatwe...fanya uungwana kwa kuirudisha simu ya watu.....ridhika na hali yako...........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…