Naomba ushauri, kuhusu elimu na maisha.

Naomba ushauri, kuhusu elimu na maisha.

Codrix

Senior Member
Joined
May 18, 2019
Posts
192
Reaction score
219
Salamu kwenu.

Mimi kwa sasa ni mwanafunzi mwaka wa 3, chuo kimoja cha taasisi ya dini, kozi ya uuguzi ngazi ya diploma ikiwa imebaki kama miezi miwili nimalize chuo kuna changamoto zifuatazo.

1. Kupungukiwa ada ya masomo, mzazi uwezo wake wa kulipa ada umekuwa ni mgumu, hana pesa maana alipoteza kazi, yupo tu kwa sasa hivyo basi maisha ya chuoni yamesogea mpaka sasa kwa mazungumzo ya mzazi wangu na chuo kuwa wavumilie atalipa, anatafuta angalau mteja wa kiwanja chake auze apate pesa lakini inachelewa maana mteja hapatikani, naelekea mwisho hivyo wanataka kulipa kwanza pesa yao ndio nitafanya mtihani wa mwisho, isipolipwa sifanyi mtihani, nadaiwa 4.3m Jumla ya ada ni 9m kwa miaka mitatu ya diploma mzazi amefanikiwa kulipa 4.7m, ili kufanya mtihani wa mwisho.

MIPANGO YANGU.

1.Niendelee kusubiri uamuzi wa chuo juu ya hatima yangu, kama wataamua nifanye mtihani ama la, endapo nikiruhusiwa kufanya mitihani na kugraduate, nitafute kazi kwa kutumia leaving certificate, endapo nikifanikiwa kupata kazi nianze kupunguza deni, mfano nikilipwa laki 2,nitumie laki moja kujikimu na laki moja nitumie kulipa ada kwa kila mwezi mpaka nitakapomaliza deni hilo nikishirikiana na mzazi, nitakapomaliza ndipo nitapata cheti changu nikitumie kuomba nafasi serikalini.

2.Nisipofanikiwa kufanya mtihani, hapa sitakuwa na leaving certificate wala document yoyote ya kunitambulisha nimemaliza chuo, nitakuwa nimepoteza miaka mitatu, hivyo sitokuwa naajirika, itanibidi nirudi kufanya kazi za kibarua, biashara binafsi hapa nimepanga nitatafuta namna ya kuweza kupata pesa nirudi tena shule nikasome kwa pesa yangu.

3.Niondoke nyumbani nikatafute popote pesa ya kuweza kukamilisha malengo yangu, muda mwingine nawaza nisipofanikiwa kufanya mtihani au kupata kazi, nisahau kabisa kuhusu mambo ya shule.nifanye maisha mengine kabisa.

*Tumejaribu kutafuta wafadhili Hatujafanikiwa
*Kusoma pia imekuwa ni changamoto maana usumbufu chuoni ni mwingi kwa ajili ya pesa yao.
*Ndugu wenye uwezo baba akiongea nao wanasema hawana kitu

Samahani mimi sio mzuri katika uandishi, naombeni ushauri wakuu maana nahisi nipo njia panda.

Shukrani
 
Poleee Mkuu ndio changamoto zetu hizo..nakutakia kila la kheri umalize Japo kwa mbinde hivyohivyo
 
Ukiwa mwanaume hiyo ni changamoto kweli kweli,kwa 'ke' angetumia fursa ya uumbaji hadi kwao angetuma matumizi;Mambo yakiwa magumu mkuu ongea na uongozi wa chuo wakupe 'option' ikiwezekana uahirishe mwaka.
 
Dahh imeniuma sana mdogo angu dahhh

Ila nikushauri kitu usisahau kusali omba kwaajili ya wazazi omba kwaajil yako naamin ipo siku haya yatakuwa ni story tu pia soma kwa bidii ukiwa na mawazo ya nje i mean elimu ya maisha naamin utafanikiwa
 
Asante sana mkuu
 
Ukiwa mwanaume hiyo ni changamoto kweli kweli,kwa 'ke' angetumia fursa ya uumbaji hadi kwao angetuma matumizi;Mambo yakiwa magumu mkuu ongea na uongozi wa chuo wakupe 'option' ikiwezekana uahirishe mwaka.
Shukrani sana mkuu kwa ushauri, option ya kuahirisha mwaka haitakuwa nzuri kwangu maana nimebakiza miezi miwili tu kumaliza, na huwa inatokea wanaruhusiwa kufanya mtihani wakiwa na na madeni, japo sio uhakika.
 
Pole sana mkuu.
Mi nilitaka nikushauri uahirishe chuo lakini nimeona hiyo option huitaki coz unaelekea kumaliza.

Sasa nakushauri uendelee kukomaa tu ukitarget hiyo bahati ya kuruhusiwa kufanya mtihani uhitimu.

Kama utapata pesa ambayo haitoshi kumaliza deni usiwape ili uje uitumie kutafuta pesa yao(mtaji)

Usitarget kuwa employed kama hutakuwa na certificate, hata hivi kwa sasa kuwa employed ni vigumu sana labda kama unauhakika tayari au una connection. Lakin kama una mpango wa kuja kitafuta kazi kwa kutuma maombi kama kina furani utajidanganya sana.
YOU WILL NOT GET EMPLOYED FOR GOOD
 
Shukrani mkuu kwa ushauri, kusema kweli option ya kuahirisha mwaka naona kama ninechelewa hivi, nimesoma miaka mitatu kasoro miezi miwili naweza nikaachia ngazi, wenzangu nyuma wakafanya mtihani, itakuwa ni habari mbaya sana hii, ngoja nikomae nao mwanzo mwisho angalau nikija kushindwa mwishoni kabisa sitajilaumu.

Kuhusu kufikiria kuwa empoyed mkuu, daah hapo pia ni pagumu ukizingatia hali ya sasa, sina connection wala kujuana na mtu yoyote.
 
Mungu akufungulie njia Kijana Mwenzangu kwa namna yoyote ile huitimu masomo yako.

Ningependa sana kukusaidia ila sina uwezo uwo but GOD IS GREAT atakujalia.
 
Asante sana, ngoja tupambanie mpaka mwisho.
 
Back
Top Bottom