Naomba ushauri kubadilisha dawa ya psoriasis

apprentice1997

Senior Member
Jun 8, 2016
107
225
Habari wakubwa, nina miaka 20 tatizo la psoriasis limeanza toka nina miaka 7 nimetibiwa hospitali nyingi ya mwisho ni agakhan dar kuna profesa alinambia kufikia miaka 18 itapungua sana, na kweli imepungua sana mwili mzima sina shida tena. Tatizo ni kuwa miezi mitatu iliyopita nilienda jkt mujibu wa sheria kutokana na kukosa usingizi imerudi tena na kwa mara ya kwanza nimepata vipele vingi usoni japokuwa havijapasuka kuwa vidonda ila mwilini imepotea baada ya kutumia dawa ila usoni bado. Sipo comfortable sana na hii hali na nataka kuondokana nayo. Ninatumia dawa ya kupaka entezma/diprosalic zamani nilikuwa natumia methotrexate na folic acid ila nimeacha sababu baada ya kusoma madhara yake. Niliwahi tibiwa na sonaderm cream zamani sana ikanisaidia nataka niijaribu, naombeni ushauri wenu kama kuna dawa nyingine nzuri ya niitumie inayoweza kupunguza hili tatizo. Asante
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom