Naomba ushauri juu ya ubora wa Corolla splinter

NDESSA

JF-Expert Member
May 2, 2013
1,946
1,791
Kuna gari tajwa hapo juu inauzwa na mm nahitaji gari naomba uzoefu juu ya aina hyo ya gari.Year of manufacture 2000.
Naomba kujua ubora/uimara wake,fuel consumption etc
 
Mkuu kama wasemea AE110 model haina hata haja ya kuuliza. Ni gari moja imara sana, spare zake bado ni nyingi sana na nafuu. Fuel consumption yake ni very friendly kama ni engine ya 5a. Kifupi ni gari roho ya paka.
Naamini hata wakija wadau wengine watakuja na positive review ya hii gari
 
Ndessa yaani hiyo iko poa mno na hasa ukiipata kwa kampuni kama autorec au trust za japan na ikawa certfied na jevic wee utalitumia mpaka unaingia kaburini
 
Mkuu kama wasemea AE110 model haina hata haja ya kuuliza. Ni gari moja imara sana, spare zake bado ni nyingi sana na nafuu. Fuel consumption yake ni very friendly kama ni engine ya 5a. Kifupi ni gari roho ya paka.
Naamini hata wakija wadau wengine watakuja na positive review ya hii gari
Upo sahihi kabsa mdau
 
Toyota nyingi ni ngumu. Balaa lipo Nissan na Mitsubishi
Sio kwamba Nissan na Mitsubishi ni mbovu au siyo imara. Shida wabongo inatuanzia kwenye bajet zetu. Unaendesha gari unapitiliza hadi 2000km za service... kwanini gari isife/sumbue?
Oil unanua zile za kupima za Temeke kule (ambazo kiuhalisia wanachemsha na kuchuja oil chafu na kufanya reparkaging)
Unataka ufunge oil filter ya 10K!!
Bush unachonga za matairi ya magari. Mafundi wenyewe wa kupapasa papasa tuuu na kufungua hiki na kile.
Sasa hapo ndio unakuta gari kama Nissan na Mitsubishi hazitaki ubabaishaji wa hivyo.
Kwa mfano Nissan wana Transmission Oil yao kabisaaa, mbongo anataka aweke transmission oil ya Total! Kisa ni bei nafuu.
Sasa unakuta Toyota hasa older generations tunazionea kwa sababu tu zinakubali huo uonevu ulioainishwa hapo juu.

Toyota za sasa hivi nazo ukimess up kidogo tu lazima ulie kama ambavyo ungelia kwa Mitsubishi na Nissan
 
Prince Nadheem! Kwa nn Toyota ivumilie lakini Nissan na Mitsubishi zisumbue?
 
I like this...very educative
 
Kuna gari tajwa hapo juu inauzwa na mm nahitaji gari naomba uzoefu juu ya aina hyo ya gari.Year of manufacture 2000.
Naomba kujua ubora/uimara wake,fuel consumption etc
Prince Nadheem
Amemaliza ukweli woote, ila ukitaka kufurahia matumizi ya mafuta kwa sprinter na kama haupo dar chukua manual gearbox mm ninayo hadi 15.5 km per litre
 
Prince Nadheem! Kwa nn Toyota ivumilie lakini Nissan na Mitsubishi zisumbue?
Ni aina ya uundaji tu ndio hutofautiana. Hata Toyoya new generations hazitaki ubabaishaji. Ndio maana hata kwenye bandiko langu nimesema hata Toyota za sasa hivi hazitaki huo ubabaishaji. Mfano mzuri ni hizi Mark 2 za 1G zilivyoonewa. Zilipokuja gari kama Toyota Progress na GX100 VVti mafundi wengi walisema ni engine mbovu. Kwanini? Hazikutaka ule ubabaishaji. Na sasa hivi wengi Brevis zinawasumbua.
Upande wa Nissan na Mitsubishi wao gari zao hazina alternative spare kama Toyota na wamekuwa very specific, ndio maana wana fluids zao
 
Back
Top Bottom