Naomba ushauri juu ya Chama cha kujiunga

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,593
Habari wa JF,

Ni matumaini yangu mpo na afya tele. Nitangulize shukurani zangu kwanza kwenu ,leo nimekuja kwenye jukwaa hili kuomba ushauri je ni chama gani cha siasa hapa Tanzania ni kizuri kujiunga nacho, chenye sera nzuri juu ya vijana, rahisi kupata uwanachama.

Naomba ifahamike kwamba kwa miongo zaidi ya miwili sikuwahi kuwa na mlengo wowote wa kisiasa, ila sasa naona si vyema kijana kuwa vuguvugu ni bora niwe moto au baridi.

Asanteni wote!
 
Heri ujiunge na ODM mana inafungua tawi tanzania hivi karibuni
 
Kama kweli unataka kujiunga na chama cha siasa cha kweli jiunge na CCM.
 
Kama unataka kufaidi keki ya taifa jiunge Na ccm, kama unataka kupigania haki Na Na usawa Wa taifa lako jiunge Na upinzani kama ACT au Chadema.lakini kuwekwa lockup Ni muda wowote
Ebu nifafanulie hapo kwenye kufaidi na kutofaidi keki ya taifa,kuna kaupendeleo gani nikiwa mwana CCM??
 
Heri ujiunge na ODM mana inafungua tawi tanzania hivi karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app
ODM kirefu chake nini mkuu,maana ndio kwanza nakisikia hicho chama,vp taratibu za kuwa mwanachama??Je kwa makao yao makuu yapo wapi???Ningependa kujiunga nacho kama kitanivutia mkuu kama ni chama kipya bila shaka kita kuwa na njaa ya kupata wanachama.
Asante
 
Kupata kadi simple tu vijana tunapewa sana vipaumbele kikubwa ni uwezo wako wa kujenga hoja
 
ama unataka siasa za uropokaji nenda upinzani kama unataka siasa safi za watu wenye akili zao nenda CCM, kuhusu process za kujiunga sijajua kwa kwel ila mm pia nna mpango wa kupata kadi ya uanachama hvi karibuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…