Naomba ushauri, eneo la mipango miji limepeita katikati ya kiwanja changu

PAMILA

Member
Mar 23, 2014
34
21
Wakuu naomba Ushauri. Nilinunua eneo mwaka Jana mwanzoni linalofikia nusu heka, square mita 1200 ! Mwaka huu mchoro wa mipango miji umetoka Mwezi February na katika mchoro huo eneo langu barabara imepita katikati ,kipande cha kulia kimeingizwa katika eneo la shule ya msingi na eneo la kushoto ndo limebaki kama kiwanja lakini likiwa limeingiliana na viwanja vingine. Je, Serikali itatulipa fidia kwa maeneo yetu yaliyopitiwa na barabara na sehemu kuchukuliwa na shule? Na nini hatima ya wale waliokwisha jenga? Naamini nitapata Ushauri wenye weledi! Asanteni
 
Back
Top Bottom