Kwanza Hongera pili pole tatu kwa umri wa miaka 6 bado anafundishika,muelekeze taratibu kwa upole na hekima kwa yale yasiokua mazuri.
Pia usimpende upendo wa kupitiliza sana utashindwa kumrekebisha.
kwa kweli upendo wangu umepitiliza, mimi nina watoto pacha wa kike tuu wawili na yeyey ni wakiume basi namuona kaka na kwa kuwa nimetoka nae mbali,sijui amejua kuwa nampenda sana, je kumchapa itasaidia?
Pole mkuu! Inawezekana ni kipindi cha mpito tu,maana kuna umri fulani watoto huwa ni watundu sana.
Ila kama utaona anaendelea kama wewe ni mkristo,jaribu kumpeleka kwenye nyumba za ibada akaombewe maana unaweza kuta we unajua unajua mtoto kumbe si mtoto na yupo hapo kwako kwa kazi maalum ! Samahani kama ntakuwa nimekukwaza kwa lugha niliyotumia ila haya mambo yapo sana tu just believe me !
sometimes viboko vinasaidia just mlee kama wengne unavyowalea ni wakwako huyo hata kama hukumbeba tumboni.usiwaze pa kumpeleka waza ufanyenin ili apunguze utundu, hata wakwako wanaweza kuwa hvyo,
kabla sijasahau hongera sana kwa kumuasili mtoto,may god bless u,ni wachache wanaweza,and plz usife moyo wala kufikiria mara mbili
Nafikiri hiyo ni stage ambayo mtoto anatakiwa kupitia maana asipopita hapo mtasumbuana akiwa mkubwa hayo mambo atafanya mwisho atatulia tu wala usijali
ila uwe unamuonya kwa mambo ambayo anayafanya
Tatizo limekuja mwaka jana na nilipojifungua watoto wangu, huyu mtoto amekuwa na vituko vya kila aina na ana utundu uliopitiliza kiasi siwezi kusema najuta ila kiukweli naumia maana sina pa kumpeleka ni wangu. kituko cha kwanza alianza kuchana magodoro anatoa ile cover ya juu mpaka apate godoro lenyewe then anakata vipisi vidogovidogo kwa kutumia mkono vinakuwa vinji vinajaa ndoo kubwa, anapenda sana kuua wadudu na kuwaweka kwenye mfuko anawazika( hili nililifuatilia nikakuta ameshazika kama mafungu manne) anaweza kuwang'ata watoto wote au kuwapiga makwenzi., ukisahau kufunga chumba anaingia anapuliza perfume zote mpaka ziishe hili la perfume amelirudia jana usiku. kwa kweli anavituko vingi sana na sijapunguza upendo kwake kiukweli tunampenda sana.
Naombeni msaada weni nimfanye nini ili aache hivi vituko?
inawezekana kabisa ni njia ya kutafuta attention kutoka kwako hasa baada ya hao watoto wapya kuingia katika familia. Wataalamu wanashauri kuwaandaa watoto kabla ya wadogo zao hawajazaliwa na wategemee mabadiliko gani baada ya wadogo zao kuzaliwa na kuwa part ya familia. Mtoto wangu wa kwanza alibadilika ghafla baada ya mdogo wake kuzaliwa, alimpiga na kumfinya mdogo wake na alikuwa na miaka miwili na miezi kadhaa. hebu fikiria mtoto wa miaka sita atafanya nini atakapoona nafasi yake imechukuliwa tena na viwatu ambavyo hajawahi kuvisikia.
soma hiyo link inaweza kusaidia personally the information did help me.
Preparing your child for a new sibling: Overview | BabyCenter