Naomba tusaidiane kufanya Testing ya Application hii (Database Application)

hbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2011
Posts
678
Reaction score
298
Habari yenu wana jamvi, tumetengeza Database application kwa ajili ya kuhifadhi taarifa za watu waliobatizwa. Mtu akibatizwa anasajiliwa kwenye database kwa kuingiza jina lake, tarehe ya kuzaliwa, tarehe ya kubatizwa na taarifa zingine kama mtakavyoziona kwenye fomu ya usajili. Lengo kubwa ni kurahisisha upatiikanaji wa taarifa za watu walibatizwa, ili kujua mhusika anaishi wapi, alibatizwa lini, mawasiliano yake, michango anayoitoa nakadhalika. Pia kuwe na uwezo wa kuprint taarifa hizo katika pdf.

Kwa sasa tumetoa version ya kwanza ya application hiyo, na tunaifanyia testing katika live server ili tuweze kuiboresha zaidi na kutoa final verison.

Naomba mtusaidie katika testing, unaweza kuingia kwenye application hiyo na kujaribu kufanya kitu kulingana na maelezo niliyotoa, kisha utueleze mapungufu utakayoyaona ili tuweze kuboresha, ikiwa ni pamoja na urahisi wa kuitumia, "response time" unaporequest kitu, na fetures zingine zozote.

Username: admin
password: admin

Bofya hapa kuingia

Asanteni sana...
 
Kitu nilichoona kinafaa kurekebisha ama kuongeza ni katika sadaka/zaka. Unaweza weka ''ahadi'' ''ahadi iliyotimizwa'' kwani sidhani kama sadaka ya kawaida huwa inakuwa monitored. Bali ahadi
 
Nimeiangalia database yenu na ni nzuri sana.

Mapendekezo:

1. Kila mtu apewe namba ya usajili (unique registration number) ambayo itatumika kama primary-keys yake.

2. Sadaka au Zaka kwa sasa zinaonyesha namba moja each (labda ni jumla). Ningeshauri mngetengeneza tables 2 (moja ya Sadaka na nyingine ya Zaka) zitakazo onyesha details za contributions kama vile, tarehe, kiasi (kilichotolewa au ahadi), dhumuni (km kumbukumbu ya mfu), n.k.. Hizi tables zitakaa kwengine na ziwe linked kwa mtoaji kupitia primary-key yake.

3. Kuwe na njia ya kumlink kila mtu na watu wengine kwenye hii database anaohusiana nao kama vile mke wake, mume wake, mtoto, n.k. through their unique registration numbers hivyo kwamba unaweza ku-generate report kwa familia au individuals.

3. Status za ndoa ziwe nne. AMEOA, HAJAOA na AMEOLEWA, HAJAOLEWA. Ukicheck jinsia kuwa ni mume basi options za ndoa ziwe mbili za kwanza, na kama ni mke basi options za ndoa ziwe the last two only.

4. Ongezeni fields za TAREHE YA NDOA, na TAREHE YA KUFA

5. Mengine baadae
 
mwanzo mzuri, hongera sana na nafurahi kuona Tanzania tunaamka kama wenzetu. Iko siku tutashangaza ulimwengu wa programming kama Poland
 
Kitu nilichoona kinafaa kurekebisha ama kuongeza ni katika sadaka/zaka. Unaweza weka ''ahadi'' ''ahadi iliyotimizwa'' kwani sidhani kama sadaka ya kawaida huwa inakuwa monitored. Bali ahadi

Asante kwa ushauri wako, lakini namna ilivyo ndivyo ambavyo wahusika walitaka iwe
 
hii dtabasu home page ya kujisajiri mbona haipo
mansakankanmusa mtu haruhusiwi kujisajili mwenyewe anasajiliwa na mtu maalum, ambaye kwa sasa ni admin, ili kumsajili mtu atabofya kwenye menu upande wakulia "Ongeza mtu" itatokea fomu kisha atajaza details zote
 
Last edited by a moderator:
1. Kila mtu apewe namba ya usajili (unique registration number) ambayo itatumika kama primary-keys yake.

Kwa sasa application inampa kila mtu namba ya usajili ambayo ni tofauti na wengine, na ndiyo inayotumika kumtofautisha na watu wengine.

Asante kwa hili, kama nilivosema awali kua hii ni version ya kwanza kabisa, baada ya kupewa mahitaji na wateja wetu, lakini katika kipengele cha sadaka na zaka tutakibadilisha, hakitakua kikionekana wakati wa kusajili bali itakua ni menu inayojitegemea. Na pia sadaka kwa jinsi walivyosema inatolewa kila jumamosi, ivyo muhusika atakua anaingiza kiasi kilichotolewa siku hiyo, na system yenyewe itakua inaongeza kiasi hicho ili mwisho wa siku ipatikane jumla ya mtu huyo kwa mwezi mzima. Pia unique id ambayo inatengenezwa wakati wakumsajili mtu ndiyo itakayosaidia wakati wa kuongeza sadaka aliyotoa

3. Kuwe na njia ya kumlink kila mtu na watu wengine kwenye hii database anaohusiana nao kama vile mke wake, mume wake, mtoto, n.k. through their unique registration numbers hivyo kwamba unaweza ku-generate report kwa familia au individuals.

Kwa hili itabidi tushauriane na wateja wetu,lakini katika version inayofuata wametuambia tuongeze kipengele cha mtu wa karibu pamoja na mawasiliano yake.
3. Status za ndoa ziwe nne. AMEOA, HAJAOA na AMEOLEWA, HAJAOLEWA. Ukicheck jinsia kuwa ni mume basi options za ndoa ziwe mbili za kwanza, na kama ni mke basi options za ndoa ziwe the last two only.

4. Ongezeni fields za TAREHE YA NDOA, na TAREHE YA KUFA

Tarehe ya ndoa tutaiongeza, tarehe ya kufa nayo tutashauruiana, kama wataona inafaa tutaiongeza pia. Asante kwa ushauri wako.

5. Mengine baadae

Asante sana kwa mchango wako, pia ukipata nafasi naomba ujaribu kumsajili mtu/watu na ufanye chochote kile ambacho utaona kinawezekana kisha utuambie ugumu au usumbufu ambao utakutana nao kama mtumiaji wa kwaida.
 
nice... ila nategea final version iwe na muonekano mzuri
 
It is a good start.Check with your validation for example your system doesnt validate dates field
 
Naomba mtusaidie katika testing.... kisha utueleze mapungufu utakayoyaona ili tuweze kuboresha.
Thank you for using Yii. I love to see yet another member from Bongo.

Sina ushauri juu ya features kwa kuwa inategemea mteja wako kasemaje but nadhani kwa kuwa unatumia Yii ungeangalia uwezekano wa kutumia Yii Booster
YiiBooster

Hii Ni forum niliyoitelekeza kwa muda (sina muda wa kuiendeleza kwa sasa) inatumia Yii na YB
 

Attachments

  • demo.png
    26.4 KB · Views: 50
kwa kuwa unatumia Yii ungeangalia uwezekano wa kutumia Yii Booster
YiiBooster
Okey mkuu shukrani kwa ushauri wako, nitajaribu kutumia kwa projects zingine.. hii kazi ilikua ya haraka sana ila tawashauri kama wakikubali kuongeza muda nitaibadilisha.. pia kwa kua actions nyingi ni za crud ninampango wa kutumia extension moja ivi nimeiona inaitwaa ajaxcrudgiitemplate.
Am in love with Yii(Yes It Is)
 
Okey mkuu shukrani kwa ushauri wako, nitajaribu kutumia kwa projects zingine.. hii kazi ilikua ya haraka sana ila tawashauri kama wakikubali kuongeza muda nitaibadilisha
Deadline headache as usual!
Developers' daily problem 🙂

.. pia kwa kua actions nyingi ni za crud ninampango wa kutumia extension moja ivi nimeiona inaitwaa ajaxcrudgiitemplate.
Am in love with Yii(Yes It Is)
Nice ext!
Thanks for pointing out! :yo:
 
hii inasaidia kitu gani naomba mnifamishe
chebi ipi iyo unayouliza? Kama ni hiyo application, ni kwa ajili ya kuhifadhi taarifa za watu waliobatizwa.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…