Naomba tafsiri ya chama kuunda serikali

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,975
8,274
Labda kabla ya kupata majibu ningependa kuonyesha namna mie ninavyoelewa kuhusu chama kuunda serikali, mie nina elewa kama ifuatavyo;

Chama cha siasa kinaposhinda uchaguzi mkuu (Raisi na viti vingi vya wabunge), Raisi wa chama husika anaunda baraza lake la mawaziri na kuteua watendaji wakuu wa idara mbalimbali nyeti pia kwa mujibu wa katiba yetu Raisi anakwenda zaidi na kuteua wasaidizi wake katika ngazi ya chini kama wakuu wa mkoa na wilaya ambao wanamsaidia raisi na kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa chama husika. Kwahiyo hapa raisi anakuwa na viongozi wa aina mbili, moja ni watendaji wa serikali ambao wanasimamia utekelezaji wa kila siku wa shughuli za serikali ambao ni mawaziri na viongozi wa serikali na pili ni watawala ambao ni wakuu wa mikoa na wilaya ambao wanasimamia au wanafuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwenye halmashauri zilizopo katika mikoa yao ambazo zinakuwa zina watendaji mbalimbali kama kulingana na wizara zetu na ambao wanasimamiwa tena na baraza la madiwani ambao ndio wanaunda halmashauri. (hii kwa mujibu wa set up ya serikali yetu labda katiba mpya ije na kitu kingine na hii ni namna navyoelewa mie labda kama kuna wazoefu wanaweza kunisaidia)

Nirudi kwenye observation yangu kama nilivyoleta heading;

Katika kipindi cha wiki hizi mbili nimeshuhudia mkutano mmoja wa viongozi wa CCM wilaya na watendaji wa serikali wa halmashauri ya wilaya ya Ilemela. Na Nape akatema cheche kwa kusema ni marufuku kwa watendaji wa serikali kukataa kuhudhuria kikao cha chama pindi wanapohitajika kwani wao ndio wameunda serikali.

Hapa ndipo nilipojiuliza tunaposema chama kuunda serikali ina maana chama kinawafuatilia moja kwa moja watendaji wa serikali kama alivyosema Nape na kama walivyofanya CCM wilaya ya Ilemela au kinafuatilia kupitia muundo wa serikali kama nilivyoainisha hapo juu? maana kama raisi ameteua safu yake ya uongozi tena ana wakuu wa mikoa na wilaya ambao kivitendo kazi yao ni kuhakikisha matakwa ya chama yanatekelezwa na bado haitoshi kuna baraza la madiwani ambalo nalo linasimamia utekelezaji wa shughuli za serikali (na halmashauri nyingi zimeundwa na CCM), sasa kwanini tena chama kinafuatilia tena direct? maana concern yangu hapa nadhani mawaziri baada ya muda flani ndio wana jukumu la kutoa report kwa chama kuelezea utekelezaji wa shughuli za serikali kisha chama kinatoa mapendekezo ya namna ya kuboresha.

Hofu yangu CCM wasipojipanga kwa hili wanaweza kusababisha migogoro maana kila kiongozi wa CCM katika ngazi zote atajiona ana mamlaka ya kumwingilia mtendaji wa serikali wakati watendaji kazi yao ni kutekeleza shughuli za serikali kama miongozo inavyotaka na kutoa report ambayo nyingine inapelekwa serikalini na kwenye chama kilichounda serikali


Wazoefu wa siasa za Tz naomba msaada wa tafsiri ya chama kuunda serikali na namna kinavyotekeleza ilani yake ya uchaguzi. Nasema hivi kwa kuwa nime-observe viongozi wa CCM wilaya ya Ilemela wakiwa na mkutano wa pamoja na watendaji wa serikali(hii haina shida sana kwangu) ila kilichonishangaza ni kauli ya Nape kusema ni marufuku kwa mtendaji wa serikali yeyote kukataa pindi anapotwa katika mkutano wa chama maana uzoefu unaonyesha wengi hukataa kuhudhuria.

Samahani naweza nikawa sijaweka katika flow nzuri ila kwa wale walioelewa wanaweza kunisaidia maana tatizo linaelekea kuota mizizi maana hata leo Geita limetokea mwenyekiti wa CCM wa Geita amekwenda kukagua mradi wa maendeleo na watendaji wa serikali na wananchi wakakabidhiwa gari la wagonjwa lililotolewa na serikali ambayo ni kodi za wananchi wote bila itikadi lakini ansimama mtendaji wa serikali badala ya kusema imeletwa na serikali yeye anasema imeletwa na CCM wakati pale yeye amesimama kama serikali ambapo anatakiwa afanye kazi pasipo kuonyesha kuelemea popote ila wenye serikali yao wanapokuwa kwenye majukwaa ya siasa baadae ndio watajinadi wameleta gari la wagonjwa

Nadhani vyama vya siasa kazi yao ni kutoa miongozo ya utekelezaji kwa serikali (Ilani) na kuunda mamlaka ambazo zinafanya ufuatiliaji mara baada ya kuunda serikali na si kufuatilia direct kama ilivyojitokeza hivi karibuni.

Wataalamu tiririkeni kwa sie tulio shallow na haya mambo tuelewe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom