Mgodo Mgodoki
JF-Expert Member
- Jul 25, 2014
- 1,399
- 1,368
Kwanini una mdanganya mwezio? Maisha ya Katavi kama Dar kwa gharama ya vyumba, chumba kizuri kuanzia elfu 30, mpaka elfu 60 inategemeana na nyumba. Na pia kwa gharama ya nyumba sio chuma, pia bei inaanzia na laki na nusu kuendelea. Kiukweli hamna tofauti na Dar hata kwa bei kilo ya nyama. Tofauti yake na Dar ni waganga wa kienyeji bei zao ni ndogo sana tofauti na wa Dar. Nasema hivi kwa sababu ndio home na pia ni mmiliki wa nyumba mbili maeneo ya kotazi jirani na shule ya msingi kashaulili.
Ila katavi ni sehemu ya watu wanaupendo sana, na ukarimu wao ni wa dhati kutoka moyon.
a moyoni
Acha kumwingiza chaka na kumuogopesha mwenzako,Maisha ya Katavi yapo chini sana kuanzia Nyumba za kupanga mpaka Lodge. Lodge ambayo hapo Dar ungelipa elfu40 hapa Mpanda Mjini ni 15elfu mpaka 20elfu. Changamoto kubwa ya Katavi/Mpanda mjini ni Migahawa/Hoteli ya vyakula vizuri maana Migahawa ya huku ni ya kiwango cha chini sana na vyakula vyao ni wali na ugali,samaki,maharage na nyama tuu hakuna varieties. Na changamoto kubwa kupita yote iliyopo hapa Mpanda Mjini ni Umeme na Maji. Umeme unaweza kukatika hata siku tatu.