Naomba sera mpya ya Elimu, 2014

Naomba sera mpya ya Elimu, 2014

Kimbori

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
6,292
Reaction score
4,785
Jana raisi alizindua sera mpya ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2015.
Kwa mujibu wa raisi, sera hiyo inalenga kuboresha elimu, baada ya kufanikiwa kupanua elimu.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi alisema kwamba sera hiyo inalenga kuwapa Watanzania maarifa ili kuchochea mpango wa maendeleo 2010 - 2025, wa Tanzania kuwa na uchumi wa kati.
Nimeitafuta sera hiyo kwenye tovuti ya wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, tovuti hiyo haifunguki, "Ministry of Education and Vocational Training This site is down for maintenance. Please check back again soon. Tovuti inafanyiwa marekebisho. Tafadhali iangalie tena muda sio mrefu".
Naomba mwenye sera hiyo aiweke humu ili wadau wengi tuangalie namna ya utekelezaji wake.
 
Rais Jakaya Kikwete leo amezindua Sera
ya mpya ya Elimu na Mafunzo ya
mwaka 2014 ambapo kwa mujibu wa
sera hiyo, pamoja na mabadiliko
mengine miaka ya kupata elimu ya awali
imepunguzwa kutoka miaka miwili hadi
mwaka mmoja.
Sera hiyo pia inapunguza umri wa
kuanza darasa la kwanza kuwa miaka
mitano badala ya miaka saba na
muundo wa elimu utakuwa ni
1+6+4+2+3+ badala ya 2+7+4+2+3+ ili
mhitimu amalize mzunguko wa masomo
kwa muda mfupi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo
uliofanyika katika shule ya sekondari
Maji ya Chai iliyoko Kiwalani jijini Dar
es salaam, Rais Kikwete amesema kuwa
lengo kuu la sera hiyo ni kuifanya
Tanzania ifikie lengo lake la kuwa Taifa
lenye uchumi wa kati ifikapo mwaka
2025.
Rais Kikwete amesema kukua kwa
uchumi na ongezeko la watu nchini
kumezua changamoto nyingi, hivyo ni
lazima elimu inayotolewa ikidhi
matatakwa ya mabadiliko huku akiitaka
wizara ya elimu kuwa na utaratibu wa
kitabu kimoja cha kufundishia kwa kila
somo nchi nzima.
Amesema kwamba utaratibu unaotumika
sasa kila shule kuwa na kitabu chake cha
kufundishia ni chanzo kikuu cha watoto
kufeli.
Rais Kikwete pia amezindua maabara za
shule za sekondari kitaifa ambapo
amesema katika kutambua umuhimu wa
elimu nchini bajeti ya wizara ya elimu
imeongezeka kwa asilimia 20.
Akizindua maabara kitaifa Rais Kikwete
amewataka viongozi ambao
hawajakamilisha ujenzi wa maabara
katika maeneo yao kuongeza juhudi
kwani kipindi cha miezi sita
alichoongeza kitaisha akiwa madarakani
hivyo hatasita kuchukuwa hatua ikiwa
ni pamoja na kuwafukuza kazi au
kutengua uteuzi.
Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi
Mh Shukuru Kawambwa amesema lengo
la kuanzisha sera hiyo ni kuhakikisha
watoto wa kitanzania wote wanapata
elimu bila ubaguzi na kwamba sera
imebainisha maeneo ambayo serikali na
wadau watayawekea mkazo zaidi ili
kutoa elimu bora.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa maabara za
shule za sekondari mkoani Dar es
Salaam mkuu wa mkoa huo Bw Said
Mecky Sadick amesema maabara 281
zenye thamani ya shilingi bilioni 10.9
zimejengwa huku mkuu wa wilaya ya
Ilala akitoa taarifa ya ujenzi wa
maabara ya kisasa iliyotumika kuzindua
maabara zote nchini.
 
Jana raisi alizindua sera mpya ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2015.
Kwa mujibu wa raisi, sera hiyo inalenga kuboresha elimu, baada ya kufanikiwa kupanua elimu.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi alisema kwamba sera hiyo inalenga kuwapa Watanzania maarifa ili kuchochea mpango wa maendeleo 2010 - 2025, wa Tanzania kuwa na uchumi wa kati.
Nimeitafuta sera hiyo kwenye tovuti ya wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, tovuti hiyo haifunguki, "Ministry of Education and Vocational Training This site is down for maintenance. Please check back again soon. Tovuti inafanyiwa marekebisho. Tafadhali iangalie tena muda sio mrefu".
Naomba mwenye sera hiyo aiweke humu ili wadau wengi tuangalie namna ya utekelezaji wake.

Hiyo Sera Mpya Nakuhakikishia Kuwa Itadumu Kuanzia Mwezi Huu February Hadi November 2015 Nikimaanisha Kwamba Ni Ya Kisiasa Zaidi Na Kulenga Kupata Umaarufu Na Ushindi Wa Kisiasa Kutoka Kwa Wale Wenye Uelewa FINYU na HABA. Chezea Revolutionary Party Wewe!
 
Sijaielewa bado hii sera, hebu mwenye document ya sera yenyewe atuwekee hapa ili tuisome na kuichambua.
 
Hiyo Sera Mpya Nakuhakikishia Kuwa Itadumu Kuanzia Mwezi Huu February Hadi November 2015 Nikimaanisha Kwamba Ni Ya Kisiasa Zaidi Na Kulenga Kupata Umaarufu Na Ushindi Wa Kisiasa Kutoka Kwa Wale Wenye Uelewa FINYU na HABA. Chezea Revolutionary Party Wewe!

Mkuu mimi pia nina hisia hizo. Hakuna utekelezaji baada ya November.
 
Jamani mwenye nayo aiweke hapa tuisome maana website yao haifunguki.
 
Tanzania is a political country but politics is not Tanzanian country
 
kikwete.jpg

Bye Std VII exams, English; Karibu Kiswahili in studies - National - thecitizen.co.tz

Yaani hiyo picha dogo anayetoa maelezo juu ya human skeleton amevaa glove moja ya pili iko wapi? Au ndio maabara kutokuwa na vifaa vya kutosha?!
 
Jana raisi alizindua sera mpya ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2015.
Kwa mujibu wa raisi, sera hiyo inalenga kuboresha elimu, baada ya kufanikiwa kupanua elimu.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi alisema kwamba sera hiyo inalenga kuwapa Watanzania maarifa ili kuchochea mpango wa maendeleo 2010 - 2025, wa Tanzania kuwa na uchumi wa kati.
Nimeitafuta sera hiyo kwenye tovuti ya wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, tovuti hiyo haifunguki, "Ministry of Education and Vocational Training This site is down for maintenance. Please check back again soon. Tovuti inafanyiwa marekebisho. Tafadhali iangalie tena muda sio mrefu".
Naomba mwenye sera hiyo aiweke humu ili wadau wengi tuangalie namna ya utekelezaji wake.

bofya hapo upakue

http://necta.go.tz/files/SERA2.pdf
 
HABARI WANA JUKWAA, BILA SHAKA NYOTE MNA AFYA NJEMA. SERA YA ELIMU ILIYOZINDULIWA JANA NA MHE: RAIS HII HAPA
SERA2.pdfView attachment 226854

Ahsante sana! Naipitia kujiridhisha mwenyewe. Kimsingi yanayosemwa yamenikwaza kwa ni ishara ya wazi ya kuangania na kuteketea kwa taifa. Nimetamani nipate mapunziko nje ya nchi ili kupunguza stress za Bongo.
 
Hiyo Sera Mpya Nakuhakikishia Kuwa Itadumu Kuanzia Mwezi Huu February Hadi November 2015 Nikimaanisha Kwamba Ni Ya Kisiasa Zaidi Na Kulenga Kupata Umaarufu Na Ushindi Wa Kisiasa Kutoka Kwa Wale Wenye Uelewa FINYU na HABA. Chezea Revolutionary Party Wewe!
Ulikua sahihi. sasa hivi Ndalichako ameiweka kapuni
 
Hiyo Sera Mpya Nakuhakikishia Kuwa Itadumu Kuanzia Mwezi Huu February Hadi November 2015 Nikimaanisha Kwamba Ni Ya Kisiasa Zaidi Na Kulenga Kupata Umaarufu Na Ushindi Wa Kisiasa Kutoka Kwa Wale Wenye Uelewa FINYU na HABA. Chezea Revolutionary Party Wewe!
mmh
 
Back
Top Bottom