Naomba niwasaidie heart broken men and women kama nilivosaidiwa mimi

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,321
11,314
Miaka inavyozidi kwenda mbele uhuru wa binadamu unaongezeka sana kutokana na sera za demokrasia na kudidimia kwa maadili ya kidini, hivyo kuwapa watu nafasi kubwa ya kuingia kwenye mahusiano mapema.

Hali hii pia imechangia kwa ongezeko la kuumizwa kimapenzi kwa watu wengi sana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo tamaa za fedha, usaliti,umbali kati ya wapenzi, shinikizo la wazazi, utofauti wa dini, mitazamo tofauti kati ya wapenzi na kadhalika.

Madhara makubwa sana yamekua yakisababishwa na hali hii ya kuachana ikiwemo watu kujiua hasa vijana, kuathirika kisaikolojia, kufeli mitihani, kuacha kazi na kupoteza muelekeo wa kimaisha kabisa.

Leo naenda kuongelea jinsi ya kumsahau mpenzi wako aliyekuacha na kuanza maisha mapya yenye furaha na amani kama zamani..

Usiyazuie machozi yako:

Maumivu haya yatakufanya ulie sana na kujilaumu kwanini ulipenda lakini ni vizuri kulia sana kadri unavyoweza kwani hii itakupa ahueni na kupunguza maumivu makali unayoyapata.

Futa namba zake:
Kuendelea kuwa na namba zakekutakufanya uendelee kumpigia ili abadilishe mawazo yake hii itakufanya uumie zaidi hasa kama hakutaki tena na huenda ana mtu mwingine badala yako. Hata kama umezikariri kichwani usiziandike tena kwenye simu yako.

Kuwa bize na mambo mengine;
Fanya mazoezi, katembelee sehemu ambazo hujawahi kwenda na rafiki zako, angalia filamu za mapigano, sikiliza miziki isiyohusiana na mapenzi. Hii itakufanya usahau mapema kuliko kukaa nyumbani peke yako na kuwaza sana kuhusu mpenzi wako.

Usifiche hisia zako:
Kama umeachwa usione aibu, ongea na ndugu na jamaa zako na uwambie ukweli kuhusu yaliyokutokea, hii itakufanya upunguze mzigo wa nawazo kichwani kwako na utahisi hali ya wepesi moyoni mwako hasa kwa ushauri utakaopata. Pia unaweza kuwaona wataalamu wa ushauri kwa ushauri zaidi.

Usitafute mpenzi mwingine kuziba pengo lake haraka.:
Watu wengi huchukua wapenzi wapya haraka ili kuzuia maumivu lakini hii sio njia sahihi kwani siku maumivu yako yakiisha utagundua kwamba hauna mapenzi ya kweli juu ya huyu mpenzi wako mpya na utaishia kumuumiza tena huyo uliyemchukua (mwanamke anaweza kujifunza kumpenda mtu lakini mwanaume asipokupenda mwanzoni hawezi kujifunza kukupenda hata iweje)

Andika mapungufu yake kwenye karatasi:
Jaribu kukumbuka matatizo na mapungufu ya huyo mpenzi wako hii itakufanya uone kwamba hakuna madhara uliyoyapata ila faida na itakupunguzia machungu yako.

Msamehe mpenzi wako ata kama hajakuomba msamaha:
Njia pekee ya kua huru kihisia ni kusamehe, visasi moyoni havitakusaidia kabisa kuondokana na maumivu na utajikuta unawaza kufanya mambo ya ajabu ambayo yanaweza kukuletea matatizo ikiwemo kumuua au kumjeruhi.

Kaa mbali na vitu vinavyokukumbushia kuhusu mpenzi wako:
Sikiliza nyimbo mpya, weka mbali picha zake na zawadi zote alizokupa, usitembelee sehemu ambazo zinakukumbusha kuhusu yeye. Kua na marafiki wapya ambao hawakumfahamu mpenzi wako (simaanishi uwaache marafiki wa zamani), pia usijaribu kua rafiki wa mpenzi uliyeachana nae kwani utajikuta unaumia zaidi labda baadae sana ukishasahau.

Usiseme mabaya kuhusu mpenzi wako au familia yake:
Hii ni hali ya mpito tu, ukianza kupost vitu vya ajabu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mahusiano yako haitakusaidia kitu bali kujiabisha kwa jamii na siku maumivu yakiisha utajuta sana kwanini uliandika mambo hayo. Hili ni tatizo sugu kwa watu wengi walioachana kupost vitu kama kumkomesha mpenzi wake wa zamani. Naomba nikwambie mapenzi hayana kisasi kama umeachwa, umeachwa tu. kumbuka silence is the best weapon..

Fikiria faida za kuishi bila mpenzi:

Kuwa peke yako kuna faida nyingi ikiwemo kuwa huru na maamuzi yako, kuchagua marafiki unaotaka, kujikinga na magonjwa ya zinaa, kuishi maisha unayotaka bila kuhofia kukosolewa, unaweza kuzima simu yako ata wiki nzima bila hofu, kulala peke yako bila bugudha, kupunguza msongo wa mawazo ambao hutokana na ugomvi wa mara kwa mara.

Tumia dawa za kupunguza mawazo;
wakati mwingine maumivu ya kuachana na mpenzi yanaweza kua makali sana, mtu akshindwa kupata usingizi, kufanya kazi zake, kukosa furaha kabisa na kulia kila siku. hii huathiri sana mfumo wa maisha husika na huweza kusababisha mtu kuamua kujiua kabisa kama mnavyosikia watu waliojiua sababu ya mapenzi.

Ndio maana kuna dawa maalumu za watu wenye msongo wa mawazo. ukitumia dawa hii mwili unatulia na ubongo unapumzika sana. itakupa usingizi na kila ukiamka unakua na furaha upya na unaendelea na maisha yako kama kawaida. Dawa hizi zinaharakisha sana kusahau na kuendelea na maisha yako haraka kuliko kujaribu kupambana mwenyewe.

Mfano wa dawa hizo ni Bupropion, Clomipramine na Doxepin. zinapatikana maduka makubwa ya madawa kwa gharama kubwa kidogo lakini ni bora kuliko kuendelea kupoteza muda kumuwaza mtu ambaye hakutaki tena kwani hiyo ni gharama kubwa zaidi.

Amini utapata mwingine;
Katika dunia hii hakuna mtu alizaliwa kwa ajili ya mtu fulani..kila mtu anaweza kutengeneza mahusiano na mtu yeyote yule na yakawa mazuri, hakutaki hakutaki tu,,he/she is not worth your pains and sorrows, there is someone out there who is worth your pains..jipe mda wa kutosha usiwe na haraka fanya mambo yako.. BELIVE ME, ANOTHER TIME WIL COME..NEW LIFE, NEW LOVE AND NEW HAPPYNESS.AND THAT WONDERFUL TIME WILL LAST FOREVER.

"""And so you know the way it feels to cry, the way that I cried when you broke my world in two, And baby I learned the way to break a heart, I learned from the best, I learned from you"""- Whitney Houston

 
you made it......

√lakini mkuu unajua unaweza sema let her/him go lakini still she/he left some good scar katika moyo ni vigumu lakini inabidi tujifunze kufanya hivyoo

√ishi ya namba hapo daa unaju wengine namba za wale tuwapendao ndo zipo kichwani mara kwa mara ,hata ukaifuta ni vigumu kuondoka katika ubongo, halafu ubongo kitu ambacho hukitaki ndo always utakikumbuka , kwa hilo asee sidhani kama itasaidia katika notion ya kumsahau

√√Wakati unaandika mapungufu yake kuna wakati hayo mapungufu yake yalimfanya yeye ajirekebishe kupitia kukufanyia mazuri either kukununulia zawadi ili kuomba samahani yani utajikuta unakumbuka mazuri yake aliyokufanyia then unaanza kutafuta mbinu za kumrudia, haya mapenzii bhanaaa
 
Nshawahi kuwa broken heart mara tatu kwa same girl I loved her too much adi alishawahi nambia xaid I don't deserve this love you gave me but yet n yet I gave her everything but I came to understand love is one of the most complicated thing you may love one who do not love you and being love by the person who do note love you but mwisho wasiku that's life n now sijui who will break my heart na ikauma sana kama ilivyomwanza I take care of my self no since I understand I am my own saviour
 
It happened to me once, after he broke the engagement, without knowing he had met someone else and they got married. I was hurt, I don't know how passed through over it. Two years after he travelled looking for me, without knowing that the marriage was on fire, kindly I told him to go.
 
It happened to me once, after he broke the engagement, without knowing he met someone else and they got married. I was hurt, I don't know how passed through over it. Two years after he travelled looking for me, without knowing that the marriage was on fire, kindly I told him to go.
Pole
 
It happened to me once, after he broke the engagement, without knowing he met someone else and they got married. I was hurt, I don't know how passed through over it. Two years after he travelled looking for me, without knowing that the marriage was on fire, kindly I told him to go.
we should learn to let them go but in love there must be torelance in any case, how many engagement would you made in case of several break up, though he went to have another engagement and yet marriage but there is still some love mark in both yours

*let him/her go is sometime happens because of extreme heart broken without knowing you still an asset to him
 
we should learn to let them go but in love there must be torelance in any case, how many engagement would you made in case of several break up, though he went to have another engagement and yet marriage but there is still some love mark in both yours

*let him/her go is sometime happens because of extreme heart broken without knowing you still an asset to him
No, after what he did there was no way I could have been an asset to him nor him to me, but we still talk as friends. His marriage didn't last and he met someone else but I refused to be that replacement.
 
Back
Top Bottom