NAOMBA NIULIZE SWALI LANGU MNISAIDIE WANASHERIA KWA VIFUNGU.

ashomile

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,625
2,443
Hivi mtu akisitishiwa mkataba na alikuwa kabakiza kama miezi sita ni lazima alipwe pesa ya mkataba wake au asilipwe maana naona makampuni mengi yakiwasitishia watu mikataba huwa yanawalipa mwezi mmoja tu mingine mitano halipwi ,hii ni sahihi kweli ?
Na hajaiba sema kavunja displinary code za kazi yake.MNISAIDIE NIELEWE NAMI MAANA NAONA JAMAA ZANGU WENGI HAWALIPWI
 
Nikuto kuamua tu kudai haki yako,ila unatakiwa punde mkataba wako wa kazi unapo vunjwa na ikiwa mwajiri wako ndiyo alie terminate unatakiwa ulipwe remedies(fidia) za damage na ni kwa kipindi chote kilichobaki mpaka pale mkataba unapoisha
 
Vzr mkuu sasa naomba unisaidie kwa vifungu
 
Inategemea na makubaliano ndani ya mkataba. kuna mikataba mingine ina kipengele ndani kinachosema "Yoyote atakae vunja mkataba huu, atamlipa mwenzake fidia yenye thamani ya mwezi mmoja tu/mshahara wa mwezi mmoja mbele".

Mingine unakuta ina kipengele "Atakae taka kuvunja mkataba huu, ni wajibu atoe NOTICE ya siku 7/masaa 24" n.k.

Kwenye kipengele cha kulipana mshahara wa mwezi mmoja mbele, hapa iwe mfanya kazi au mwajiri akiuvunja basi atamlipa mwenzake mshahara wa mwezi mmoja.

Mfano,

Tuseme "wewe" ni mwajiriwa wa JF (mfanya kazi) halafu JF ndio mwajiri wako, ikitokea wewe umepata kazi sehem nyingine yenye maslahi mazuri zaidi, halafu mkataba wako wa JF una miezi 10 mbele, ila hichi kipengele kipo katika mkataba wenu. Basi wewe utamlipa JF (Mwajiri wako) thamani ya mshahara wako wa mwezi mmoja. Na kama yeye akitaka kuvunja huo mkataba nae atakulipa wewe mshahara wa mwezi mmoja.

Kuna mikataba mingine ina kipengele cha kulipana mpaka "thamani ya mwaka mmoja". Inatofautiana na makubaliano baina ya MWAJIRI na MWAJIRIWA.
 
Barikiwa kwa maelezo ya kinaga ubaga
 
Back
Top Bottom