Naomba nisaidiwe juu ya hili

Naomba nisaidiwe juu ya hili

makua

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2013
Posts
208
Reaction score
40
Habari zenu wanajamvi!

Mimi ni kijana (mvulana), ninaelimu yangu ya kuungaunga, nimegraduate mwaka 2011 kozi ya utunzaji kumbukumbu ngazi ya cheti (certificate of records management)

Nimefanya kazi kwa ujitolea kama mtunza kumbukumbu msaidizi kwa mda wa miezi kumi yaani january-october, 2012

Baada ya kuona maisha yanazidi kuwa magumu nikaamua niache kazi kwani nilikuwa nafanya pasi kulipwa hata kidogo, ndipo nikaanza kutengeneza sofa, nilikuwa nafanya katika ofisi ya mtu kwa makubaliano anilipe kila kazi nayofanya, mwanzoni tulienda vizuri ila mwishoni pakawa na mabadiliko, katika kazi tano,ananilipa mbili zingine halipi, nikaamua niache.

Nikawa nahamasisha baadhi ya vijana ambao ni mafundi wa sofa ili tuungane na tufungue ofisi kubwa ambayo itakuwa miliki yetu hivyo tutaepukana na manyanyaso ya mabosi, ila waliishia kuitikia bila utekelezaji...

Kwa sasa lengo langu ni kufungua ofisi yangu ya kutengeneza sofa na kuziuza, natumaini nikifanikiwa basi nitatengeneza ajira zisizopungua tatu. (mafundi wawili na muuzaji mmoja)

OMBI
1: Kwa sasa naomba nipate kibarua chochote chenye kunipatia kipato ambacho nitaweza kufikia malengo yangu.

2: Nimetembelea baadhi ya taasisi za kifedha ili nipate mkopo ila nimeshindwa kupata vigezo vya kukopa.
Kwahiyo kama kuna mtu ambaye yukotayari kunisapoti kivyovyote basi nahitaji msaada.

3: Kama kuna mafundi wa sofa au wenye uhitaji wa fundi humu basi naomba kampani yenu tuwepamoja ili maisha yaendelee..nipo tayari niishi mahali popote duniani ilimradi maisha yaende.

Naishi Dar es salaam, Magomeni.

Nawasilisha
 
Kwanza hongera kijana kwa jinsi unavyofight. Pili, pole kwa kudhurumiwa. Tatu, nakutia moyo-endelea kupambana. Kwa macho ya imani nakuona ni mtu fulani tajiri na mheshimiwa ajaye soon and very soon.
 
Kwanza hongera kijana kwa jinsi unavyofight. Pili, pole kwa kudhurumiwa. Tatu, nakutia moyo-endelea kupambana. Kwa macho ya imani nakuona ni mtu fulani tajiri na mheshimiwa ajaye soon and very soon.

Ahsante
 
Ok, hebu naomba uwe muwazi, ni mtaji wa kiasi gani unaoweza kukusaidia kuanza hiyo biashara???????
 
Hiyo kazi unayoomba ukiipata seem utaiacha pia kwa kuwa CV yako inaonesha una experience ya kuacha kazi mara kwa mara!
 
Hongera sana ila me naona mtangulize mungu utafanikisha mungu nimuweza wa yote.
 
Ok, hebu naomba uwe muwazi, ni mtaji wa kiasi gani unaoweza kukusaidia kuanza hiyo biashara???????

1milion nafiliri inanitosha...

Matimizi kwa hiyo pesa ni..

1: Kupata fremu nitakayoitumia kama duka (showroom)

2: kununua baadhi ya vitendea kazi kama cherehani na stappler

Ni hivyo tu kwa kuanzia.
 
Hiyo kazi unayoomba ukiipata seem utaiacha pia kwa kuwa CV yako inaonesha una experience ya kuacha kazi mara kwa mara!

Kwa kawaida tunafanya kazi kwaajili ya maendeleo na sio maonesho hicho ndicho kinanifanya niwe naacha kwani sioni maslah upande wangu ndio maana natafuta kilicho bora..
Siachi kwa uzembe mkuu
 
Hongera sana ila me naona mtangulize mungu utafanikisha mungu nimuweza wa yote.

Naami hivyo,kwa mungu kilakitu chawezekana najuhudi zinahitajika...
Ahsante mkuu
 
hongera sana kijana utajiri upo machoni pako...pole kwa yaliyokukuta ..napenda watu wanaoona mbele kama wewe..vijana wengi wakishasoma na kuwa na degree zao hawqtqki kuziweka chini kabisa na kuangalia plan B wao ni appliication tuuu..nitakupm kijana
 
Nakutangulizia shukrani.....
Nitashukuru sana
 
Mkuu naona kama tunaweza kuunganisha nguvu ndg yangu!
kama hujapata mdau anae eleweka basi nicheki asbh tuone chakufanya na ntajtahdi mtaji+pakufanyia kazi ninapo ila upcountry na biashara ya sofa inalipa sana pande hizi.
 
Ok ngoja nikufuate piem mkuu.
 
Umenifurahisha unavyopigana natumai utafanikiwa cos hakuna ajuaye kesho yke kla k2 kitakuwa sawa.
 
Back
Top Bottom