Naomba mwenye uelewa anisaidie kuhusu ada ya chuo ninachosoma

Wile king

Member
Jun 15, 2016
10
2
Ndugu zangu wanaJF, ninaomba mwenye uelewa kuhusiana na hili swala anisaidie nilielewe. Nitajaribu kulielezea mpaka pale uelewa wangu utakapokwamia.

Katika kipindi cha nyuma, ulipaji wa ada katika chuo fulani ulionekana mzuri na uliokuwa unazingatia utofauti wa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo na wa pili.
Katika ulipaji huo nitatumia kilichokuwa kinaitwa "other fees" kuonesha ni jinsi gani ulipaji wake ulizingatia utofauti kati ya mwanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili.

Other fees. (214,000)
Haya ni malipo aliyokuwa akifanya mwanafunzi mpya/ mwaka wa kwanza. Anapoingia mwaka wa pili, malipo haya yalipungua kutokana na ukweli kwamba baadhi ya vipengele vyake vilitolewa once. Mfano ni kitambulisho cha mwanafunzi. Hichi kitakutambulisha kwa muda wako wote wa masomo mpaka unapohitimu. Yapo mengine tofauti na kitambulisho, hivyo hakukuwa na sababu ya kulipia tena pale unapoingia mwaka wa pili.
Sababu hizo zilifanya ulipaji wa "other fees" kutofautiana baina ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo na wa pili.

Kwa sasa hali imebadilika kwani hakuna tena cha mwaka wa kwanza au wa pili, wote mtalipa sawa.

Medical fee.
Hili ni swala lingine ambalo malipo yake kidogo yanachanganya watu.
Unapokuwa na bima ya taifa bado inakuwa ni lazima ulipe sh 50,000 na unapewa bima ya chuo yenye category b. Kiukweli hakitusaidii lolote kwani ukiumwa ukaenda katika hospitali yao hutapewa huduma yyt.

Kwa wale wasio na bima ya taifa malipo yao ni sh 100,000 na wao ni kweli kwamba wanapata huduma zote ktk hospitali ya chuo.
Utata wangu ni kwamba, kama nina bima ya taifa na huduma zangu napata kwa kutumia bima hiyo, kwanini iwe ni lazima kulipa tena sh 50,000 ikiwa sipati huduma yeyote chini ya bima yao ya category b ninapougua?

Mwenye kujua chochote embu tusaidiane.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom