Naomba msaada waharaka ZIP/POSTAL CODE ndio nini?

Naomba msaada waharaka ZIP/POSTAL CODE ndio nini?

Mfano Mimi nipo mwanza ntatumia postcode. Ya mwanza au lazima niwe na box langu
Kwa jinsi ninavyoelewa mimi, kukizungumzia huduma za posta duniani (katika huduma ya barua) basi postal code,post code,zip code na pincode vyote ni kitu kimoja sema majina tu yametofautiana katika nchi mbalimbali. Neno postal code hutumika sana canada, zipcode hutumika sana marekani na ZIP ni kifupi cha Zone Improvement Plan na hili neno pincode hutumika sana nchini India ambapo PIN ni kifupi cha Postal Indexing Number.
Sasa hizi code husaidia katika usambazaji wa barua kuweza kutambua kiurahisi eneo gani ambapo barua inabidi ipelekwe na kwa mara nyingi (hutegemea na nchi) hii code huwa inaandikwa baada ya sanduku la posta kuandikwa.. Kwa nchi kama india sijawahi kuona kama wanasanduku la posta lakini wao wana ofisi kubwa za posta katika maeneo mbalimbali kwahiyo kinachotokea ni kwamba barua ikitumwa kwa mfano ije dar basi itaandikwa dar es salaam lakini hii code itawekwa ili watu wa posta waweze jua ni ofisi zao zipi zipo karibu na eneo husika barua inahitajika kufika. sasa kama barua inatakiwa ifike mwenge basi code ya mwenge itawekwa alafu wale watu wa posta mwenge watajua kuwa address iliyotajwa juu ni ya sehemu gani pale mwenge..je ni makongo au mlalakuwa au hapo TRA n.k..
natumai nimeeleweka..
kama kuna mtu hajanielewa asisite kuuliza na tutasaidiana kuelewa kadiri ya upeo wetu..
nashukuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom