Naomba msaada wa ushauri kuhusu mahusiano yangu

debbug

JF-Expert Member
Jun 9, 2018
391
500
Wakuu habari za muda huu. poleni na pia hongereni kwa majukumu ya kila siku

Samahani mimi sio mwandishi mzuri kwaiyo kwa wale wote mtakao kerwa na uandishi wangu misamehe sana .Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada

Mimi mdogo wenu nihitaji sana mawazo yenu na ushauli wenu .Story ni kwamba nilikuwa na mahusiano na binti fulani tangu mwaka 2018 lakini mahusiano yetu yalikuwa sio imara sana kutokana na huyu binti kutokuwa sereous sana na mimi .Na muda wa mahusiano yetu hatukuwai fanya kitu chochote kutoka na binti kwanza alikuwa anasoma form six na hakutaka tufanye chochote na alidai ni bikra

Lakini baadae huyu binti alimaliza shule na kujiunga na chuo kikuu dar (jina kapuni ) na kipindi icho mimi ninakaa moshi.Mwezi wa 12 mwaka jana nilipata safari moja ya kwenda dar na nikamwambia na baada ya kumwambia tukakubalia kwamba nikifika nita spend nae siku zote nitakapo kua uko.Kweli tulikutana na tukawa pamoja kwa muda wa siku nne

Baada ya wiki mbili kupita nilivyo rudi moshi huyu binti akanambia hazio siku zake na amaeenda kupima umekutwa anamimba ya wiki mbili basi mikamwambia pow inabidi ujifungue akakubali lakini akasema sitaki kuendelea kukaa chuo kwasababu kwanza ni fedhea pili siwezi kusoma nikiwa na mimba kwaiyoa nataka kuja kwako .Mimi nikamkatalia sana nikwamwambia jitahidi kusoma ivyo angalau ufanye kitihani ya first semister ndio uje lakini akagoma sana sana basi akasema nimtumie nau ili aje na kweli nikamtumia nauli na akaja

Baada ya kuja sasa nikamwambia naitaji ndugu yako yeyote ajue kuwa tupo wote ili nisije ingia sana kwenye matatizo na ndugu zako dah akagoma kata kata akasema anaplan zake kwaiyo atakiwi mtu yeyote kujua mpaka atakapo jifungua .Basi kila nikimkumbushia kuhusu ilo swala tunagombana sana na pia wakati amefika akaniorodheshea kila vyakula anavyo vihitaji kweli nikajitahidi nikanunua kila alichohitaji ili awe anapika ndani sasa cha ajabu ni kwamba tangu nimenunua ivyo vitu hapiki kazi yake ni kucheki season kutoka asubui mpaka usiku njaa ikimuuma kuna sehemu nimezoea kuacha pesa kwa shida yoyote itakayo jitokea sasa yeye anachukua iyo pesa nakwenda kununua chips tu

nikimwambia basi safisha ata ndani hataki ,basi pika hataki yaan wakuu kazi zote nafanya mimi na kula ninakula nje na mimba ndio kwanza inamwezi mmoja tu kwaiyo matatizo ni mawili yaan hataki ndugu zake wajue pili yaan hafanyi chochote ndani na hivi ninavyoongea tangu asubu alipo amka ni muvi tu mpaka usiku huu nimeamua kuzima tv na kaanza kulia ety na mnyanyasa kwasababu anashida sasa wakuu naomba ushauri mdogo wenu nini nifanye kuhusiana na hali kama hii
asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Stephen Chelu

Verified Member
Oct 31, 2017
4,569
2,000
Huwa nasikia kuna mimba huja na kisirani kwa mhusika, ila akili yangu inakataa kukubali hilo katika hili kwa sababu ulishasema kuwa huyo binti hakuwa serious na mahusiano kuanzia awali hivyo inaonekana atakuwa bado katika mwendelezo wake na sasa ana nguvu kubwa kwa kuwa ana mimba. Kuwa mvumilivu, halafu utumie akili yako binafsi kujua nini lengo la huyo binti katika mahusiano yenu.

NB: ukiona mtu haeleweki tangu mwanzo wa mahusiano usijipe moyo kuwa atabadilika siku za usoni, achana nae. Kujaribu kumvumilia kunaweza kusababisha matatizo makubwa mbeleni.
 
Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
29,536
2,000
Unajipalilia makaa kukaa na mwanamke bila ndugu zake kujua..tena ana ujauzito!
Usiendeshwe na mwanamke, piga hata makofi akuonyeshe ndugu zake wakufahamu!
Utajuta baadae(Ila ni kawaida kwenu watu wa kaskazini kuwa chini ya mwanamke )
 
Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
25,863
2,000
Mdogo wangu, hapo bado haujapata mke aiseeee....
Na usije ukajilazimisha kumuoa mwanamke kwasababu tu eti unamhurumia, pia nikukumbushe kwamba kuzaa nae sio sababu ya kutosha basi awe mke wako.
Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sinyora

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
779
1,000
simama kama mwanaume huyu mwanmke atakuendesha na amejua udhaifu wako unampenda sana alf kakuaa na mtu katika hali hiyo bila kwao kujua ni hatari sana
 
Sang'udi

JF-Expert Member
May 16, 2016
2,397
2,000
Mkuu,

Usikae na mtoto wa watu bila ndugu zake, hasa wazazi wake, kujua. Lisipotokea tatizo hakuna shida, lakini ikitokea tatizo utafanyaje?

Hatuombei iwe hivyo, lakini assume akikata ukiwa naye, nani atakuelewa? Fanya mpango ndugu zake wajue.

Otherwise unajitafutia matatizo.
 
Davey 2017

Senior Member
Mar 24, 2017
108
250
Mimi nafikiri tatizo ni choices zako, you choose kuwa naye, you choose kupelekwa na you are still choosing tabia mbaya zake. Dogo hebu ukirudi home mpe two options Option 1. unataka awajulishe wazazi wake na aende huko kwanza na uilee mimba na mtoto wako mahusiano yavunjike ama Option 2, Awajulishe wazazi wake na abadilike siku zote za maisha yenu ndipo uwe tayari kuwa naye kumlea mimba na mtoto wako

All in all kuwajulisha wazazi wake siyo optional, hawezi aende popote atakapojisikia, hataki andaa mkwanja nije na wazazi wake.

Pia nitumie namba zako nikufundishe mambo ya kusimama kama mwanaume kwenye mahusiano
 
Gyole

JF-Expert Member
Sep 20, 2013
6,908
2,000
Huyo ni kimeo, mimba wk 2 tu aache chuo? Una uhakika alikuwa anasoma? Una uhakika mimba Ni yako? Je Ni kweli ulimtoa bikra? All in all huyo hafai hata kwa bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DiasporaUSA

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
22,848
2,000
Wakuu habari za muda huu. poleni na pia hongereni kwa majukumu ya kila siku

Samahani mimi sio mwandishi mzuri kwaiyo kwa wale wote mtakao kerwa na uandishi wangu misamehe sana .Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada

Mimi mdogo wenu nihitaji sana mawazo yenu na ushauli wenu .Story ni kwamba nilikuwa na mahusiano na binti fulani tangu mwaka 2018 lakini mahusiano yetu yalikuwa sio imara sana kutokana na huyu binti kutokuwa sereous sana na mimi .Na muda wa mahusiano yetu hatukuwai fanya kitu chochote kutoka na binti kwanza alikuwa anasoma form six na hakutaka tufanye chochote na alidai ni bikra

Lakini baadae huyu binti alimaliza shule na kujiunga na chuo kikuu dar (jina kapuni ) na kipindi icho mimi ninakaa moshi.Mwezi wa 12 mwaka jana nilipata safari moja ya kwenda dar na nikamwambia na baada ya kumwambia tukakubalia kwamba nikifika nita spend nae siku zote nitakapo kua uko.Kweli tulikutana na tukawa pamoja kwa muda wa siku nne

Baada ya wiki mbili kupita nilivyo rudi moshi huyu binti akanambia hazio siku zake na amaeenda kupima umekutwa anamimba ya wiki mbili basi mikamwambia pow inabidi ujifungue akakubali lakini akasema sitaki kuendelea kukaa chuo kwasababu kwanza ni fedhea pili siwezi kusoma nikiwa na mimba kwaiyoa nataka kuja kwako .Mimi nikamkatalia sana nikwamwambia jitahidi kusoma ivyo angalau ufanye kitihani ya first semister ndio uje lakini akagoma sana sana basi akasema nimtumie nau ili aje na kweli nikamtumia nauli na akaja

Baada ya kuja sasa nikamwambia naitaji ndugu yako yeyote ajue kuwa tupo wote ili nisije ingia sana kwenye matatizo na ndugu zako dah akagoma kata kata akasema anaplan zake kwaiyo atakiwi mtu yeyote kujua mpaka atakapo jifungua .Basi kila nikimkumbushia kuhusu ilo swala tunagombana sana na pia wakati amefika akaniorodheshea kila vyakula anavyo vihitaji kweli nikajitahidi nikanunua kila alichohitaji ili awe anapika ndani sasa cha ajabu ni kwamba tangu nimenunua ivyo vitu hapiki kazi yake ni kucheki season kutoka asubui mpaka usiku njaa ikimuuma kuna sehemu nimezoea kuacha pesa kwa shida yoyote itakayo jitokea sasa yeye anachukua iyo pesa nakwenda kununua chips tu

nikimwambia basi safisha ata ndani hataki ,basi pika hataki yaan wakuu kazi zote nafanya mimi na kula ninakula nje na mimba ndio kwanza inamwezi mmoja tu kwaiyo matatizo ni mawili yaan hataki ndugu zake wajue pili yaan hafanyi chochote ndani na hivi ninavyoongea tangu asubu alipo amka ni muvi tu mpaka usiku huu nimeamua kuzima tv na kaanza kulia ety na mnyanyasa kwasababu anashida sasa wakuu naomba ushauri mdogo wenu nini nifanye kuhusiana na hali kama hii
asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
Vumilia

Hizo ni side effects za mi m mba mkuu
 
Tuttyfruity

JF-Expert Member
Dec 3, 2017
1,849
2,000
1.Je ni kweli alikuwa bikra na uliitoa bikra yake?
2. Hiyo mimba umejiridhisha ni yako(nahisi mtego upo hapa)?
3. Hana mpango wa kuendelea tena na chuo?
4. Naomba umri wenu ili niweze kuwashauri

Sent using Jamii Forums mobile app
Maswali muhimu sana.

Anyways back kwa mtoa mada miaka yote mna "date" hujui hata rafiki yake? Hamna mtu anaejielewa anaweza kuacha chuo kisa mimba. Huyo sidhani kama alikua anasoma.

Hapo kwako anakaa kwa misingi ipi?
1. either anakupenda na anataka kua na wewe in which case angeishi na wewe kwa upendo na heshima including kukusaidia kazi za ndani na kujisaidia mwenyewe 2. Anatafuta tu hifadhi alee mimba mpaka itakapo kua kubwa na kujifungua (ukute mwenye mimba kaikataa hana pa kwenda).

Hiyo mimba ina wiki anazosema? Nenda hospitali kampime kipimo cha B-hcg kinaonyesha mimba ina muda gani.

Anyways hapo huna mke. huyo ni housemate.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom