Naomba msaada wa tatizo la kucheua mara kwa mara

Naomba msaada wa tatizo la kucheua mara kwa mara

LHFT

New Member
Joined
Mar 4, 2011
Posts
4
Reaction score
2
Wana Jamii,

Nina tatizo la kucheua mara kwa mara. Na haswa pale ninapotoka kula naweza kupata tatizo hilo hata kwa masaa matatu. Nilichogundua hadi sasa ni kuwa chakula ninachokula hakisagiki mapema hivyo kupelwkwa kucheua harufu kali ya chakula kama vile nimekula mda huo huo.

Nimeshindwa kujua tatizo kuu linatokana na nini. Kwani nimeahajaribu kula kidogo ila bado hali inaendelea. Pia nimebadili vyakula ila nafuu ipo kidogo. Kwani siwezi kuacha kula baadhi ya vyakula kwani kipato nacho hakiruhusu.

Naombeni msaada kimawazo ni nini tena naweza kufanya. Hospitali waliniambia nina gesi nyingi na walitaka ninywe dawa kwa muda mrefu
 
Jaribu kuepuka
  • Vyakula vyenye mafuta mengi,
  • Vyenye viungo vingi,
  • Kunywa vinywaji vyenye gesi nyingi kama soda,epuka kahawa na chai pia
  • Milo mikubwa
  • Sigara
  • Mienendo yako ya kula.Kula taratibu usiwe na papara.
  • Kulala baada ya mlo
Una tatizo linaloitwa acid reflux/regurgitation.Una sababishwa na muscle iliyopo kati ya tumbo na lower oesophagus sphintcher(LES) kulegea,kutokufunga sawa sawa, au kufunguka kwa sana.Hii inaweza kusababisha maumivu kwenye kifua au kiungulia na vilevile kucheua sana.Dalili nyingine unazoweza kuwa nazo ni kama
  • Kwikwi
  • kichefchef
  • Damu kwenye choo kikubwa
  • Kupoteza uzito bila sababu
  • Koo kuwa kavu au kuwa na maumivu kwenye koo kwa muda mrefu
Tatizo hilo linaweza kutatuliwa na antacids(MgOH,Al[SUB]2[/SUB](OH[SUB]3[/SUB])/acid neutralizers kama bicarbonates (Na[SUB]2[/SUB]CO[SUB]3[/SUB]/MgCO[SUB]3[/SUB]) au Histamin [SUB]2[/SUB] resptor antagonists(rantidin) au Protonpumpinhibitor(osemeprazol,esomeprazole)
 
Nabeua kila mara na kifua kubana.

Moyo unadunda kwa nguvu nausikia mpaka miguuni. Sijui nifanyeje
 
Namimi muhanga jamnani mwenye kujua dawa atusaidie maumivu nimakali sana
 
Jaribu kuepuka
  • Vyakula vyenye mafuta mengi,
  • Vyenye viungo vingi,
  • Kunywa vinywaji vyenye gesi nyingi kama soda,epuka kahawa na chai pia
  • Milo mikubwa
  • Sigara
  • Mienendo yako ya kula.Kula taratibu usiwe na papara...
Hiyo ni dalili ya ugonjwa unaoitwa gerd, ambao husababishwa na ulcers, nenda hospitali haraka sana
 
Back
Top Bottom