Naomba Msaada wa mbinu za kukuza na kuendeleza biashara

Entreprenuare

JF-Expert Member
Aug 24, 2019
1,616
1,714
Wadau mambo vipi?

Nadhani kila mfanyabiashara anapenda kuona biashara yake inakuwa kila siku, au kila baada ya muda fulani, hapa nina maanisha kwamba , kama ulianza kuuza chapati 20 kwa siku, basi tuna tegemea baada ya muda fulani uweze kuuza chapati 50 kwa siku.

Sasa, wataalam wa biashara na wazoefu, naomba mnipe mbinu za kukuza na kuendeleza biashara fulani,
 
Biashara ya bar
Hakikisha usafi wa mazingira hasa chooni na wahudumu wawe na lugha yenye staha.
Usalama wa mteja nao pia ni mhimu kuna bar zingne yaani kuumizana ni dakika 0 , mziki nao ni kivutizi tosha kwa wanywaji lazima wateja uwasikilize wazee tuwekee bolingo kina shala mwana kina Franco kina madilu kina msondo n.k vijana wakipga kelele wawekee matusi yao maana sku hizi syo nyimbo tena.
 
Kwanza kabisa jitahidi kujua target ya biashara yako, ni ngumu sana kwa biashara kumfaaa kila mtu kwa wakati mmoja..

Kama ni bar weka mazingira mazuri, mziki mzuri (hapa hakikisha Dj wako anaweza kwenda na moods za wanywaji, wakiwa bia hazijakolea na zikiwa zimekolea), wahudumu wawe na lugha nzuri. Mengine cheza vizuri na hesabu zako, make sure kila baada ya wiki unapiga tathmini ya faida na hasara ili kujua kama unaenda mbele au unarudi nyuma.

Mengine nature itaamua ila Hard work siku zote huwa in pay.

Thank me later
 
Back
Top Bottom