Naomba msaada wa kueleweshwa kuhusu RC kutembea na mabaunsa siku hizi

Bahimba

JF-Expert Member
May 8, 2013
510
346
Kwanza tupeane pole kwa kila mmoja wetu kwa pilika pilika za hapa na pale, za kusongesha gurudumu la maendeleo, baada ya hapo naomba msaada juu ya hiki kinachonichanganya kwa sasa,

Toka kizungumkuti cha taja taja ya wahusika wa ngada, hali ya ulinzi ya mkuu wa mkoa imebadilika sana, Mh amekua akitembea na mabaunsa ambao wanakuwa nae popote anapokwenda, na wengine anakua nao kwenye gari, wengine wana gari yao, sasa maswali yangu ni haya,

1,hao mabaunsa ni moja ya askari wa kwenye majeshi yetu,,,?
2, ni walinzi wake binafsi na kama ni wake binafsi wana lipwa na nani..?
3, Na kama ni moja ya askari wa kwenye majeshi yetu je, ni wakuu wote wa mkoa wamewekewa ulinzi huo....?

Naomba wataalamu wenye weredi wa maswala ya ulinzi, naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom