NAOMBA MSAADA WA KISHERIA

NAOMBA MSAADA WA KISHERIA

Mr.MONDO

Member
Joined
Nov 4, 2015
Posts
17
Reaction score
0
Ndugu wanajamii wenzangu mimi mfanyakazi katika kampuni moja ya kimataifa(sitoitaja jina) nimefanya kazi kwa zaidi ya mwaka mmoja bila ya kupewa mkataba licha ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa na elimu ya kutosha(Shahada ya kwanza) pamoja na uzoefu.Nimeshuhudia watu wakitoka nje ya nchi wakipewa mikataba na mishahara minono licha ya kutokuwa na elimu pamoja na uzoefu hata kidogo na wengine huwa ninawafundisha kazi mwenyewe.
Nimeshajaribu kuwakumbusha mara kadhaa lakini hakuna dalili na muda niliopoteza ni mwingi na kwa sasa nafikiria kuchukua hatua zaidi hasa za kisheria ila siwezi kufanya haya bila ya kupata mwongozo kutoka kwa watu wenye utaalamu wa haya masuala ya sheria hasa zinazohusiana na mambo ya ajira,mikataba katika ajira..
NAOMBENI USHAURI NDUGU ZANGU
 
Sizan km sheria itakusaidia hpo zaid utafukuzwa kazkbsa kwasbb hun mkataba.. ushaur ongea na boss wako vzr pengn utendaj wko hauwaridhish ..au tafut kaz ingn
 
Watakuja mkuu , endelea kuwasubiri,

Jamani msaidieni mwenzetu huyo.

Nilidhani haya ma kampuni ya kimataifa ndio yanajali haki za wafanya kazi kumbe tena ni sawa huku huku tulipo sisi,
 
Back
Top Bottom