Naomba msaada wa elimu ya kodi

Naomba msaada wa elimu ya kodi

Strong ladg

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
407
Reaction score
1,054
Ndugu wataalamu, kuna mdogo wangu yuko chuo anaanzisha biashara ya kuuza vitu mtandaoni. Kila kitu tayari hadi usajili wa Brela (kasajili jina la biashara). Ishu ipo kwenye masuala ya TRA, TIN Number n.k. Kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa mtu ambaye mauzo yake kwa mwaka ni chini ya milioni 4 halipi kodi, pia mdogo wangu hatarajii kwa sasa kuweza kuingiza milioni 4 kwa mwaka.

1. Je atatakiwa kulipa kodi? ( Labda sheria zimebadilishwa)
2. Anavyoenda TRA ajipange vipi kwa usalama wa biashara yake inayoanza?

Ushauri, ukosoaji, maoni yanakaribishwa. Asanteni
 
Walipa kodi wamepungua kwa mjibu wa takwimu, hivyo ajipange kulipa kodi. Ambayo ni kuanzia 250,000(sina uhakika sana) kwa anae anza biashara. Baada ya mwaka inaongezeka au atabaki palepale kulingana na assessment au efd receipts kama atakuwa anatoa.
 
Hiyo 25000 ndo atalipa mara nne ili kwa mwaka iwe jumla laki moja ?
 
Anauza online? Hana duka au ofisi? Kama ndio, basi hakuna kodi zaidi ya labda ya kodi za serikali za kurusha matangazo au kodi za serilikali za umiliki wa mitandao kama youtube channel.

Kama atakua na ofisi, basi anapaswa kuwa na tin, atafanyiwa tathmini kujua kama mauzo yake kweli ni chini ya 4m kwa mwaka. Kama ndio basi hatalipa kodi ila atapewa kitambulisho maalumu. As time goes by, anaweza kujikuta anaanza kulipa
 
Hana ofisi, Asante sana.
 
Back
Top Bottom