Naomba msaada: TRA wamenikadiria kulipa kodi kubwa kuliko uwezo wa biashara

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,978
5,025
Ninafanya biashara ya reja reja sehemu ninayoishi, nauza nguo za watoto.
Mwaka huu TRA wamenikadiria kulipa kodi kubwa Kuliko uwezo wa biashara ninayoifanya.
Mtaji ulioabdikwa kwamba ndio uko Kwenye mzunguko ni Kama Mara tatu ya mtaji halisi. Walikadiria tu kama kawaida yao.

Niliandika barua kwa meneja kuomba kukadiriwa upya jibu nililopewa ni Kama ushauri WA nguvu za Giza.
Kwanza nilipelekwa tena Kwa wanaohusika na makadirio alipofika Kule akanambia unachotakiwa ni kulipa kodi tu.
Hayo mengine ntajijua mwenyewe.

Nimefikiria hata kuwaandikia barua ya kufunga biashara hivyo waniondoe Kwenye list ya walipa kodi kwa sasa.

Naombeni ushauri, kuna hatua gani nyingine naweza kufanya??
Natanguliza shukrani.
 
Bado nasubiria ushauri wenu ndugu zangu.
Cc mods, any jukwaa naweza pata ushauri!!
 
Mmh pole sana!!! Kuna rafiki yangu nae yamemkuta hayo. Kaamua kufunga tu biashara.
Subiri waje wakuoe ushauri mkuu!
Na Mimi option niliyonayo kichwani Ndio hii.
Maana Naona wanataka niwe natoa hela Kwenye mshahara kulipa kodi ya biashara.
 
Mkuu upo mkoa gani wa TRA ...sidhan kama huu udhalimu wa hv bado upo TRA ni kweli TRA wanafigisufigisu zao ila si za kukukadiria mara 3 Ya mtaji wako ...Jaribu kutembelea dawati la Elimu kwa mlipa kodi lipo takriban kila TRA ofisi kwa msaada zaidi
 
Kama ni mfanyabiashara mkubwa Fanya kitu kinaitwa tax appeal, ndo njia pekee, ila unaifanya ukiwa tayar umeshalipa kodi, wanakurudishia kodi iliozidi hakuna namna nyingne ndugu TRA sio mchezo, waweza fungu kweli ukapata hasara
Fanya jambo moja tu, lipa kodi then kata rufaa.
Fuata tax appeal procedures
Waone tax consultant wakujitegemea
 
Usifunge biashara kwani utazidi kupunguza idadi ya Walipa kodi, na ni juzi tu Kamishna aliongea kwa uchungu kuhusu idadi ndogo ya Walipa kodi.
 
Tafuta wataalamu wa mahesabu ya kodi watakusaidia kupangua hayo makadirio na kuwa ya wastani mkuu.Pole sana
 
Kodi ya pango unalipa kias gan? Hyo nayo huwa inaangaliwa kwenye ukokotoz
 
Mkuu TRA awana huruma kabisa....TRA vingunguziti ukienda kulipa kodi unakaridiwa then ikipelekwa kwa kiongozi wa juu anarudi kwa yule alie kukaridia anamwambia Aongeze kodi......imenifanya nifunge biashara zangu nyingi tu.

pia imenifanya nijuwe ni kwann waTanzania Wengi huwa hawalipi kodi.
 
Hahaaa nyingi ngapi mkuu? Sasa unaishije? Aisee ila kusema ukwel purchasing power iko chini ila msururu wa kodi ndio usiseme, sijui kwa sasa ila mfano mwaka 2014 kulikuwa na kodi zifuatazo;

1. Kodi ya fremu/pango
2. Kodi ya mapato (TRA)
3. Kodi ya biashara ya halmashauri
4. Kodi ya kizimia moto/fire extinguisher
5. Kodi ya mlinzi kila mwezi
6. Kodi ya usafi/ gari la taka kila mwez
7. Kodi ya maji ya bomba unalotumia hapo dukani
8. Gharama za mfanyakazi (mshahara)
Nk nk kwa mfumo huo kutoka yataka janja janja nyingi
 
Waombe formula ya kukadiria hicho unachokitaka ambayo inaonesha kila step na msingi wa kila step. Kama wakikataa basi hapo hapafai.
 
In
Ninafanya biashara ya reja reja sehemu ninayoishi, nauza nguo za watoto.
Mwaka huu TRA wamenikadiria kulipa kodi kubwa Kuliko uwezo wa biashara ninayoifanya.
Mtaji ulioabdikwa kwamba ndio uko Kwenye mzunguko ni Kama Mara tatu ya mtaji halisi. Walikadiria tu kama kawaida yao.

Niliandika barua kwa meneja kuomba kukadiriwa upya jibu nililopewa ni Kama ushauri WA nguvu za Giza.
Kwanza nilipelekwa tena Kwa wanaohusika na makadirio alipofika Kule akanambia unachotakiwa ni kulipa kodi tu.
Hayo mengine ntajijua mwenyewe.

Nimefikiria hata kuwaandikia barua ya kufunga biashara hivyo waniondoe Kwenye list ya walipa kodi kwa sasa.

Naombeni ushauri, kuna hatua gani nyingine naweza kufanya??
Natanguliza shukrani.
Nichek Inbox
 
Back
Top Bottom