Naomba msaada nimepoteza hisia

Naomba msaada nimepoteza hisia

Amos David Mathias

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2022
Posts
1,575
Reaction score
3,106
Napenda kuwasalimu wanajamii forums.Kama mada inavyojieleza hapo juu tatizo lilianza kama mafua makali ambayo yalikuwa yanafanya Pua langu liume na nishindwe kulala Kwa raha.Lakini namshukuru Mungu nilipona hayo mafua sasa kilichokuja kutokea ni kwamba nimepoteza hisia za kusikia harufu yoyote . Mwanzoni nilidhani ni kawaida kutokana na sababu nilikuwa na mafua lakini sasahivi Sina mafua na ni wiki ya SITA inaisha siwezi kuskia harufu ya kitu chochote.

Nimejaribu kujipulizia perfume Kali puani lakini bado siskii, nimejaribu kunusa haja nikiwa chooni siskii chochote, nimejaribu kunusa matawi ya miti yenye harufu Kali lakini bado siskii harufu yoyote, nimejaribu kunusa harufu Mbaya zozote unazojua lakini siskii Chochote, nimejaribu kunusa sabuni zenye manukato mazuri na zenye harufu Kali kama Rungu Bado siskii harufu yoyote, nikipika chakula siskii kama kinanukia ,nashindwa kutambua kama chakula kimevunda au Bado ni salama kula, nimejaribu kunusa KITUNGUU swaumu na Cha kawaida lakini bado siskii harufu yoyote.Na hapo nimehitimisha Kuna tatizo katika mfumo wa pua langu.

Ni ajabu Kwa sababu sijawahi ona tatizo kama hili.Naamini Kuna watu mnaelewa au mlishawahi patwa na tatizo kama hili .Naombeni msaada wenu hisia zangu za kunusa zirejee Tena .Huu sio utani ni kweli .Naomba msaada.
 
Likely uliugua Covid.

Kama jibu ni ndiyo basi hiyo ni athari mojawapo. Kuna ambao huisha haraka na kuna wengine hali hiyo inabakia kwa muda mrefu mpaka hata miaka miwili.
 
Hizi thread zingine bana....
Yaani ulivyo andika heading nimekuja nduki nikafungua chap, kuja kusoma uzi nimejikuta nachoka akili tu.
Anyway, pole
 
Napenda kuwasalimu wanajamii forums.Kama mada inavyojieleza hapo juu tatizo lilianza kama mafua makali ambayo yalikuwa yanafanya Pua langu liume na nishindwe kulala Kwa raha.Lakini namshukuru Mungu nilipona hayo mafua sasa kilichokuja kutokea ni kwamba nimepoteza hisia za kusikia harufu yoyote . Mwanzoni nilidhani ni kawaida kutokana na sababu nilikuwa na mafua lakini sasahivi Sina mafua na ni wiki ya SITA inaisha siwezi kuskia harufu ya kitu chochote.

Nimejaribu kujipulizia perfume Kali puani lakini bado siskii, nimejaribu kunusa haja nikiwa chooni siskii chochote, nimejaribu kunusa matawi ya miti yenye harufu Kali lakini bado siskii harufu yoyote, nimejaribu kunusa harufu Mbaya zozote unazojua lakini siskii Chochote, nimejaribu kunusa sabuni zenye manukato mazuri na zenye harufu Kali kama Rungu Bado siskii harufu yoyote, nikipika chakula siskii kama kinanukia ,nashindwa kutambua kama chakula kimevunda au Bado ni salama kula, nimejaribu kunusa KITUNGUU swaumu na Cha kawaida lakini bado siskii harufu yoyote.Na hapo nimehitimisha Kuna tatizo katika mfumo wa pua langu.

Ni ajabu Kwa sababu sijawahi ona tatizo kama hili.Naamini Kuna watu mnaelewa au mlishawahi patwa na tatizo kama hili .Naombeni msaada wenu hisia zangu za kunusa zirejee Tena .Huu sio utani ni kweli .Naomba msaada.
Kitaalamu una anosmia.
Huwa inaenda inapotea yenyewe.
Lakini vema ukamuone ENT kwa msaada zaidi.
 
Back
Top Bottom