Naomba msaada jinsi ya kuendesha biashara ya conference facilities

Mopalmo

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
533
138
Wana jf,ninaomba kwa anayefahamu jinsi ya kuendesha biashara ya conference facilities, ninachotaka kujua pamoja na mambo mengine ni je ninawezaje kupata tenda zake bila kuwa na ukumbi,mimi nina vifaa vya kisasa vya music ambavyo vinafaa kwa kazi hiyo
 
Unamaanisha conference kupitia video streaming,ambapo unahitaji internet connection?
 
mkuu hivi kuwa na vifaa kama hivyo unatakiwa uwe na sh ngapi??
 
ili kupata tenda ingawa huna ukumbi, kwanza jaribu kujuana na watu mashuhuri ambao wanahusika na masherehe mbalimbali ili kuwa na partnership ktk kupata tenda even jaribu kuwa mtafiti wapi kutakua na sherehe ili kuwatafuta wanakamati ili kuwashawishi wakupe tenda na ukishapata inabidi utumie hiyo chance kujitangaza zaidi! Utafanikiwa
 
Kwa kuanzia ungetafuta "event planners" wa kuungana nao ili wewe uwapatie equipment wakati unajenga network yako. Pia usidharau the power of word of mouth. Badala ya kutoa mchango kwenye sherehe za wenzio, jitolee muziki na hivyo vifaa vyako. Kama gharama ni mf laki 2, wewe unaweza kusema utatoa laki 1 na nyingine kamati itoe ili vyombo vyako vitoke... sasa hapo kazi kwako kuhakikisha vifaa vina namba yako na jina la biashara yako ili mwenye kutafakari shunguli in the near future achukuw kirahisi.

Pia makampuni ya maekrting and events promotion ni mazuri kwa kuanzia. Again, kama unajitangaza kupitia vyombo vyenyewe na quality ni nzuri, next time wateja wataanza kukutafuta wenyewe. Kila la heri!
 
Mamaee na wengine nashukuru kwa ushauri wenu nitaufanyia kazi
 
Back
Top Bottom