Mr Suprize
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 857
- 937
Habari wadau! (Mtanisamehe kwa maelezo yangu marefu)
Mimi ni kijana wa umri wa miaka 21 ..nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo la chunusi kwa takribani miaka 3 na nusu sasa.. nimewahi kwenda kwa daktari wa masuala ya ngozi kueleza tatizo langu aligundua ngozi yangu INA mafuta mengi usoni akanishauri niende duka la vipodozi nikanunue vipodozi vinavyoendana na ngozi yangu pamoja na Sabuni ya kuoshea USO wangu. pia alinishauri niende pharmacy nikanunue cream inaitwa benzoly peroxide, nilifanya hivyo nikaitumia ndani ya mwezi mmoja ngozi ilionekana kuwa na maendeleo mazuri lakini badae hali ya chunusi ikawa inajirudia tena kwa kasi ya ajabu huku nikiendelea kuitumia hiyo cream.
Baada ya kuona hivyo nikaacha kutumia ile cream nikaenda duka la vipodozi nikashauriwa nitumie ZOA ZOA lotion pamoja na Sabuni yake nikafanya hivyo lakini maendeleo ya ngozi yangu yakaja muda mfupi na kurudi katika hali ya zamani. kuna baadhi ya marafiki zangu wakanishauri nitumie betasol cream na Sabuni ya liwa nilifanya hivyo lakini mabadiliko yanakuja muda mfupi na kuacha. pia wapo walionishauri nitumie sonadem cream hata hivyo haikuweza kusaidia ..
Kiukweli tatizo hili linatesa hasa kazi ninayofanya ni ya kuonana na watu wengi muda wote wa kazi (am a teacher)
nakosa amani ninapokuwa kazini.
Naomba kwa yeyote anayejua suluhisho la tatizo langu anisaidie kwa sababu naogopa kuzidi kuharibu ngozi yangu kwa kutumia vipodozi vingi katika USO mmoja..
Naamini humu ndani kuna watalamu hata wenzangu waliowahi kukumbwa na hili tatizo.
kwa sasa nipo sumbawanga unaweza kunishauri nitumie dawa,mafuta au lotion ambayo italeta matokeo chanya katika ngozi yangu..
Natanguliza shukrani zangu.