Dear Great thinkers!! Budget mama (ya Mkulo) imepitishwa. Ndani yake kuna hii ya Ngeleja iliyokataliwa. Ngeleja atatengeneza nyingine ambayo itawakilishwa bungeni, na hii mpya lazima itakuwa tofauti sana na ilyokataliwa (ambayo imo ndani ya ile ya Mkulo). sasa hapa itakuwaje: bajeti mpya ya Ngeleja itaingiaje ndani ya ile ya Mkulo?? Ikiingizwa ndani ya ile ya Mkulo na kuifanya iwe mpya, je ya Mkulo itabidi ipitishwe upya?? Au itakuwaje?? Nielimisheni tafadhali.
Ahsante sana
Hivi ule Muswada wa Fedha (The Finance Bill) ulishapitishwa au utapitishwa baada ya Mkulo kufanya marekebisho ya Bajeti yake?Mkulo hasomi bajeti nyingine kinachofanyika ni kuhamisha mafungu ya pesa kutoka kwenye bajeti ileile ya Madini na nishati ili mafungu hayo yatumike kwenye umememe. Mfano pesa zilizotengwa kwa ajili ya Poasho,Usafiri,Magali,Utafiti, Masurufu,Mafuta zote hizo zitahamishiwa kwenye umeme. Kwa kawaida Serikali huwa haifuti kodi hata kidogo inachokifanya ni kuihamisha kodi.Mfano wakipunguza kwenye Sigara ujue wameongeza kwenye Mafuta.
Waziri Mkullo mwishoni kabisa ataleta marekebisho baada ya bajeti ya wizara zote kupita. Bajeti ya wizara ya maji nayo tunatarajia itakwama tu. Na Mwandosya mwenyewe bado yuko India.
Ule ulishapita. Pengine JK kwa sababu ya kuzurula kwake hajapata muda akausaini. Ndege ya Mkapa inamzingua ile mbaya.Hivi ule Muswada wa Fedha (The Finance Bill) ulishapitishwa au utapitishwa baada ya Mkulo kufanya marekebisho ya Bajeti yake?
Yuko India. Mgonjwa. Tatizo la maji Dar litampa taabu kwelikweli. Mh Mnyika hatamwachia kirahisi.
Mwandosya yupo India! Mbona walikuwa watowa taarifa humu kuwa ndie aliyekuwa ananunuwa madiwani wa CDM Mbeya last two days?
Kama alivyosema Mnyika jana nje ya ukumbi wa Bunge. Inabidi CDM wakomae irudishwe ili ijadiliwe upya, pia ile ya Mpango wa miaka mitano nayenyewe itakuwa imevurugika. Kazi kwelikweli.Dear Great thinkers!! Budget mama (ya Mkulo) imepitishwa. Ndani yake kuna hii ya Ngeleja iliyokataliwa.
Ngeleja atatengeneza nyingine ambayo itawakilishwa bungeni, na hii mpya lazima itakuwa tofauti sana na ilyokataliwa (ambayo imo ndani ya ile ya Mkulo). sasa hapa itakuwaje: bajeti mpya ya Ngeleja itaingiaje ndani ya ile ya Mkulo?? Ikiingizwa ndani ya ile ya Mkulo na kuifanya iwe mpya, je ya Mkulo itabidi ipitishwe upya?? Au itakuwaje?? Nielimisheni tafadhali.
Ahsante sana
Fanya hesabu rahisi; Kama ilikwisha pitishwa na inatokana na kupitishwa kwa bajeti za wizara zote, je bajeti za wiraza zote zikipitishwa na marekebisho yake ina maanisha nini?
I mean kama ulikubali kumempereka mwanao shule alipofika mwaka wa pili karo ikapanda kulinganisha na pale na ulipofanya maamuzi ya kumsomesha unafanya nini? unamwondoa shule au unaendelea kumsomesha hadi amalize masomo yake? Bajet kuu ni indications kama ingelikuwa sivyo kusingi kuwepo na bajeti za kila wizara, hivyo kupishwa kwake ndio kusema walipitisha development indicators and policies na wanapokuja kujadili bajeti za wizara wabunge wanaenda mbali zaidi kuangalia uhalisia na matarajio ya bajeti mama, what are strategies behind the indicators, wizara ina mipango gani, mbinu gani, mikakati gani etc etc, naona wewe unawaza fedha tu? bajeti siyo fedha peke yake fedha ni kiashiria tu? siyo halisi hata kidogo.
Ule ulishapita. Pengine JK kwa sababu ya kuzurula kwake hajapata muda akausaini. Ndege ya Mkapa inamzingua ile mbaya.